Maisha yao yamgubikwa na kitendawili wanajitahidi kulima na kupata mazao ya kibiashara lakini wanakwamishwa na miundo mbinu mibovu na hivyo kujikuta wakiendelea kuishi maisha ya kubahatisha pamoja na tunu ya ardhi yenye rutuba waliyonayo inayotoa mazao ya kila aina.
Hilo linasababisha baadhi ya wakulima wa bidhaa za matunda kama vile ndizi waishie kuuza kwa bei ya chini ili angalau waweze kujikimu kimaisha na hata kumudu kusomesha watoto, bali iwapo kungekuwa na mbinu mbadala za kuboresha miundo mbinu, wangeweza kusafirisha mazao yao nje ya maeneo wanayolimia na kunufaika kwa rasilimali walizonazo.
Mahitaji ya wakazi wengi wa maeneo ya vijijini hukutana na changamoto ambazo utatuzi wake ni kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya wananchi na kuona kuwa kuwepo kwao katika mfumo kumetokana na wananchi hao.
Post a Comment