Viongozi hawa enzi hizo wakiwa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini walikuwa hivi na walishirikiana kwa hali na mali katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya nchi yetu yanasonga mbele chini ya serikali ya Awamu ya Pili.
Aidha viongozi hawa kwa pamoja waliweka nia yao ya kuwania Urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005 na mchuano wao ulikuwa mkali na hatimaye JK aliibuka kidedea na Profesa Mwandosya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Dkt. Salim Ahmed Salim.
Uwajibikaji wa Profesa Mwandosya ulimfanya ateuliwa katika Baraza la Mawaziri ndani ya serikali ya Awamu ya Tatu na hata serikali ya awamu ya Nne inayoongozwa na swahiba wake JK, hata hivyo siasa za makundi ziliwageukia wapambe wa viongozi hawa na kuleta dhana ya mtafaruku ambao viongozi wenyewe hawana imani nao.
Imejengwa dhana kwa wengi kuwa JK hapikiki chungu kimoja na Prof Mwandosya!! na hii ni dhana yenye lengo la kujenga chuki miongoni mwa maswahiba hawa ilhali wenyewe wako makini katika kuwatumikia wananchi.
Prof. Mwandosya kwa sasa yupo nchini India akiendelea na matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment