|
|
Hatimaye Dereva Aden Mwampyate(55) aliyenusurika kifo Januari
19 baada ya gari alilokuwa akiliendesha kugongwa na lori na yeye kubanwa katika
msukano huku akiwa amejeruhiwa vibaya amesema kuwa anamshukuru Mwenyezi Mungu
kwa kumnsuru na kifo.
Bw. ambaye amelazwa katika hospitali teule ya Ifisi iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya anasema kuwa hakutarajia kupona kutokana
na mazingira ya ajali yalivyokuwa na kuwa kutokana na eneo alilopatia ajali
anawashukuru wasamaria waliojitokeza kuokoa maisha yake.
‘’Sikujitambua kabisa nilikuwa nasikia sauti kwa mbali hakuna
niliyeweza kumtambua siku hiyo nawashukuru sana ndugu zangu,’’alisema Bw.
Mwampyate.
Aidha Mwampyate anasema kuwa taarifa zaq tukio la ajali yake
zilikuwa zinafuatiliwa na ndugu yake aliyoko nchini Marekani aliyemtambulisha
kwa jina la Ambakisye Mwakyusa ambaye alifuatilia blogi hii na kuwajulisha
ndugu na jamaa wa hapa nchini.
‘’Ambakisye aliangalia moja kwa moja kupitia mtandao hatua
kwa hatua tangu nimepata ajali hadi nafikishwa hospitali, akaanza kuwajulisha
ndugu na jamaa nakushukuru sana ndugu yangu umenisaidia kuwajulisha ndugu zangu
kupitia mtandao wako, Mungu akubariki sana,’’anasema Mwampyate akimshukuru
mwandishi wa blogu hii.
Naye mke wa Mwampyate aliyejitambulisha kwa jina la Jenifer
anasema kuwa alipata taarifa kupitia simu ya mkononi ya mwandishi wa blogu hii ambapo mara baada ya
kupata ajali alichukua simu ya majeruhi na kutafuta namba za ndugu zake na
kupiga ili kuwajulisha ajali hiyo.
‘’Nakushukuru sana kaka yangu Mungu akubariki hatuna cha
kukulipa Mungu mwenyewe ndiye anajua umetusaidia sana,’’alisema Jenifer huku
akilengwa machozi ya matumaini.
Kwa upande wake Muuguzi mkuu wa hospitali ya Ifisi Bi. Roda
Kisongwa anasema kuwa majeruhi huyo alivunjika mguu wa kulia ambapo walimuwekea
mawe mazito baada ya kumfanyia upasuaji na kumuweka vyuma pia walimshona nyuzi
18 katika majeraha ya kichwani ambayo kwa sasa yameanza kupona.
‘’Tunawashukuru sana kwani mlifika kwenye eneo la tukio kwa
wakati muafaka hakuna alichopoteza pamoja na fedha zake zilikuwa salama
kabisa..Mungu awabariki sana vijana,’’alisema Muuguzi huyo.
Bw. Mwampyate alipata ajali baada ya gari lake kugongwa na
Lori lililokuwa likielekea Mbeya na yeye akielekea mjini Tunduma katika eneo la
Senjele ambapo mara baada ya kugongana uso kwa uso lori hilo lilipinduka
barabarani na gari lake lilitumbukia korongoni huku akiwa amebanwa na katika
msukano.
Wasamaria wema ambao walikuwa ni abiria katika Coaster
lililokuwa likielekea Mbeya walishuka katika gari hilo na kutoa msaada kwa
kumnasua katika gari na kumkimbiza katika hospitali ya Ifisi.
(Blogu hii inawashukuru jamaa wote waliochangia kwa namna
moja ama nyingine kuokoa maisha ya dereva huyu ikiwa ni pamoja madaktari na
wauguzi wa hospitali teule ya Ifisi)
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ifisi Roda Kisongwa na mke wa Aden Jenifer wakimfariji mgonjwa katika wodi ya hospitali teule ya Ifisi |
Dereva Aden akionesha mguu uliovunjika mara tatu katika ajali iliyotokea eneo la Senjele Januari 19 wakati akisafirisha gari kuelekea Tunduma |
Siku aliyopata ajali wauguzi na wasamaria wema walimsaidia kumuwahisha hospitali na kupata tiba |
Wasamaria wema walipokuwa wakimnasua siku alipopata ajali |
Post a Comment
New comments are not allowed.