Akizungumza wakati
akimkaribisha Waziri Nahodha ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa
CCM,Mwenyekiti wa CCM kata ya Tunduma Bw. Daniel Mwashiuya alisema kuwa kuna
kundi la watu wachache ambao wamejipanga kuvuruga amani katika mji huo kwa
kisingizio cha siasa.
Bw. Mwashiuya
alisema kuwa CCM iko imara katika kukabiliana na vurugu hizo ambazo zinatishia
amani na utulivu wa watu na mali zao.
Akizungumza katika
mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na kundi la wanachama wa CCM Bw.Nahodha
alisema kuwa amejionea mwenyeqwe hali ya uvunjifu wa amani na kwamba kwa kuwa
yeye ndiye Waziri mwenye dhamana ya ulinzi wa wananchi na mali zao hawezi
kufumbia macho ambapo alimuagiza Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kushughulikia
hali hiyo ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku biashara haramu eneo hilo.
Tukio la aina hii
katika eneo hilo ni la tatu ambapo tukio la kwanza lilikuwa ni wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2009 uliolazimika kubadilisha njia wakati yalipotokea
mauaji ya mfanyabiashara wa mjini Tunduma ambapo mtu wa tatu kukutana na zahama
ya kuzomewa alikuwa ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa katika
ziara ya kampeni za uchaguzi mwaka 2010.
Post a Comment