WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA PROFESA JUMANNE
MAGHEMBE AMEELEZWA KUSABABISHA MKUU WA WILAYA YA MBOZI BW.GABRIEL KIMOLO
KUJIUZULU WADHIFA WAKE WA MKUU WA WILAYA KUTOKANA NA KITENDO CHAKE CHA
KUENDELEA KUKUMBATIA BAADHI YA
WAFANYABIASHARA WANUNUZI WA KAHAWA AMBAO WAMEKUWA WAKISEMA KWAMBA HAWAZUNGUMZI
NA MBWA BALI WANAZUNGUMZA NA MFUGA MBWA.
KUJIUZULU KWA BW.KIMOLO AMBAYE AMEKUWA NI MKUU WA WILAYA YA
KWANZA NCHINI KUAMUA KUACHIA WADHIFA HUO KWA KIPINDI CHA ZAIDI YA MIAKA 20 KWA
AWAMU ZA UONGOZI WA SERIKALI YA CHAMA TAWALA KUMESABABISHWA NA SABABU ALIZOELEZA
KUWA AMEKOSA USHIRIKIANO NA WIZARA YA KILIMO KUHUSU MSIMAMO WAKE WA KUPINGA
UNUNUZI WA KAHAWA MBIVU RED CHERY AMBAYO INAFANYWA NA BAADHI YA WAFANYABIASHARA
WANAOPATA RIDHAA YA KUNUNUA KUTOKA WIZARANI.
JANUARI 17 MWAKA HUU WAZIRI WA KILIMO NA USHIRIKA PROFESA
MAGHEMBE ALIKUTANA NA BAADHI YA WAKULIMA NA WADAU WA ZAO LA KAHAWA AMBAPO
MSIMAMO WA SERIKALI ULIELEZA KUWA HAWAKO TAYARI KUENDELEA KUWAONA WAKULIMA
WAKIUZA KAHAWA MBICHI KWA WACHUUZI HALI AMBAYO BW. KIMOLO ALISEMA IMESABABISHA
YEYE KUONEKANA KUTOTHAMINIWA MSIMAMO WAKE NA WA SERIKALI YA WILAYA YA MKOA.
KADHALIKA KATIKA MAELEZO YAKE YA KUJIUZULU BW.KIMOLO ALISEMA
KUWA KWA MUJIBU WA UTARATIBU WA UTEUZI WA UNAOFANYWA NA RAIS YEYE UTEUZI WAKE
ULIANZIA MWAKA 2006 NA KUKOMA MWAKA 2010 AMBAPO HADI SASA HAKUNA UTEUZI MPYA
ULIOFANYWA NA RAIS JAMBO LINALOMFANYA ASHINDWE KUPANGA MIKAKATI YA KAZI KWA
MAENDELEO YA WILAYA YAKE.
ALISEMA KUWA, HIVI SASA NI MWAKA MMOJA NA NUSU AMEKUWA
AKIFANYA KAZI KWA MATUKIO YA DHARURA NA MAAGIZO KUTOKA JUU NA HIVYO KUMFANYA
AONEKANE KUTOWAJIBIKA VILIVYO KATIKA NAFASI YAKE NA KWAMBA AMEAMUA KUJIUZULU
AKIAMINI KUWA UAMUZI WAKE UTALINDA HESHIMA YAKE.
AIDHA AINAELEZWA KUWA BW.KIMOLO AMEKUWA NI MTU WA KARIBU
SANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU BW. EDWARD LOWASSA NA KWAMBA KITENDO CHAKE CHA
KUJIUZULU KINA BARAKA KUTOKA KWA KIONGOZI HUYO MSTAAFU AMBAPO KATIKA ZIARA YAKE
ALIYOIFANYA HIVI KARIBUNI WILAYANI MOMBA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA ALITETA
NAYE JAMBO MUHIMU.
HATA HIVYO TETESI ZA KUTOKUWEMO KATIKA UTEUZI UJAO
ZINAELEZWA KUWA NI MOJA YA SABABU ZILIZOMFANYA MKUU HUYO KUACHIA NGAZI MAPEMA
ILI KUJIJENGEA MAZINGIRA YA MAANDALIZI YA KUIKUBALI HALI HIYO KABLA HAIJATOKEA
WAKATI WA UTEUZI AMBAO UNATARAJIWA KUFANYWA NA RAIS WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA.
ALIFAFANUA KUWA KUMEKUWA NA UBABAISHAJI KWA BAADHI YA
VIONGOZI NA KUSABABISHA SERIKALI IONEKANE INASHINDWA KUWATUMIKIA VYEMA WANANCHI
NA KWAMBA YEYE AMEAMUA KUACHIA NGAZI NA ANAKWENDA KUSHUGHULIKIA MAMBO YAKE
BINAFSI.
ALIPOTAKIWA KUELEZA KAMA DHAMIRA YAKE ITAJIKITA ZAIDI KATIKA
SIASA ALISEMA KUWA WAKATI UKIFIKA KUINGIA KATIKA MCHAKATO WA KISIASA ATAFANYA
HIVYO KWA KUWA YEYE KAMA MTU YEYOTE ANA UAMUZI WAKE.
‘’NIMECHOSHWA NA KEJELI NA MIZENGWE DHIDI YA SERIKALI..WAFANYABIASHARA
WANADILIKI KUSEMA KUWA HAWAKO TAYARI KUZUNGUMZA NA MBWA BALI WANAZUNGUMZA NA
WENYE MBWA, SIWEZI KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA YA AINA HII, WANANCHI WAELEWE
HIVYO,NITABAKI KUWA RAIA MWEMA NA MWANANCHI WA KAWAIDA KAMA WENGINE.’’ALISEMA
BW.KIMOLO.
ALIFAFANUA KUWA AMEMUANDIKIA BARUA RAIS, WAZIRI MKUU NA MKUU
WA MKOA WA MBEYA KUMJULISHA HILO NA KWAMBA HUO NI UAMUZI WAKE BINAFSI NA JIBU
LOLOTE HALITABADILI UAMUZI WAKE ALIOAMUA KUUCHUKUA.
Post a Comment