Ads (728x90)



SERIKALI mkoani  Mbeya, imeshangazwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Bw. Gabriel Kimolo kutangaza hadharani juu ya kujiuzulu kwake ilhali alikuwa akijua wazi kuwa hayumo katika orodha ya wakuu wa wilaya wapya watakaoteuliwa na Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo alasiri Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro  kuwa kitendo cha Mkuu huyo kutumia vyombo vya habari kutangaza kujiuzulu ni kujikosha kwa jamii kwani anajua wazi kuwa hayumo ndani ya orodha ya wakuu wa wilaya wapya.

Bw. Kandoro alisema kuwa Mkuu huyo wa wilaya alimfuata ofisini kwake Machi 24 na kumueleza kuwa amepata taarifa za kutokuwemo katika orodha ya wakuu wa wilaya wapya hivyo anashangazwa na kitendo hicho kwani anaamini hakupaswa kujiweka hadharani na kulaumu makampuni.

Alisema kuwa kulingana na taarifa za Mkuu huyo ni kwamba alifika ofisini kwake na kumueleza kuwa alipata taarufa hizo Machi 23 kutoka katika idara inayohusika kwamba jina lake halimo.

Bw.Kandoro alisema kuwa katika maelezo yake mkuu huyo alikuwa akilalamika kwanini ameachwa wakati yeye ni mtendaji mzuri kwa wilaya na Taifa.

Alisema kuwa alichokifanya ni kujikosha kwa jamii ili isishangae wakati uteuzi mpya wa wakuu wa wilaya utakapotangazwa na kwamba Bw. Kimolo hakupaswa kuyatupia  lawama na kwamba anapaswa kukubali matokeo ili aweze kuondoka kwa amani.

Kadhjalika alimtaka kuacha kuyapaka mayope baadhi ya makampuni kwamba yamehusika kwa namna moja ama nyingine juu ya kudorora kwake kuhusu utendaji wake kudorora.





Post a Comment