Ads (728x90)
BAADHI YA WANANCHI WAKISHUHUDIA MAJERUHI WA AJALI


LORI LILILOSABABISHA AJALI NA KUUA WATU WATANO NA KUJERUHI WENGINE 130


(

(STORI NA RASHID MKWINDA PICHA KWA HISANI YA KAMANGA)

WATU watano wamekufa na wengine 130 kujeruhiwa  katika ajali mbaya iliyohusisha lori la mwekezaji kampuni ya Kapunga lenye namba za usajili T 398 BSE aina ya TIPER SCANIA kupinduka katika kijiji cha Matebete wilayani Mbarali leo asubuhi.

Lori hilo lilikuwa limebeba vibarua ambao walikuwa wakienda kupalilia katika shamba la Mpunga na mwekezaji huyo ililopo katika kijiji Mapogoro ambapo miongoni mwao walikuwepo baadhi ya wanafunzi walioacha shule na kwenda kufanya kibarua katika shamba hilo.

Mashuhuda wa ajali hiyo waliofika eneo la tukio walidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Lori kufukuzana na mwendesha pikipiki aliyekuwa amelipita gari hilo hivyo alianza kushindana nalo ili alipite.

Aidha waliokufa katika hiyo wamedaiwa kuwa ni watu watano wawili wakiwemo mwanamke na mwanaume waliofia Hospitali ambapo kamanda Athumani alipata taarifa za vifo vya watu watatu waliokufa  papo hapo katika ajali.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amesema kuwa  ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:15 asubuhi ambapo dereva wa Lori  hilo aliyefahamika kwa jina la Baraka Molel(29)  alikuwa katika mwendo kasi.

Amewataja watu waliokufa katika ajali kuwa ni pamoja na Samwel Mapugilo(30) mkazi wa Ilembula,Ben Mfupa(27) mkazi wa Mapogoro na Edgar Mwakipesile(35)mkazi wa Nonde Jijini Mbeya.

Kamanda Athumani amesema kuwa wakati gari hilo linakwenda vibarua waliokuwemo ndani ya gari hilo walikuwa wakishangilia hivyo kusababisha dereva huyo kuongeza mwendo na kusababisha ajali hiyo.

Kamanda Athumani amesema kuwa watu 130 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambapo baadhi yao wamelazwa katika hospitali ya Misheni Chimala wakiwemo wanaume 89  na wanawake 41 ambapo kati yao wanaume 49 na wanawake 25 na majeruhi wengine 56 wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein Kifu walikuwa ni miongoni mw amashuhuda wa ajali hiyo ambao walifika katika hospitali ya Misheni Chimala na kushuhudia umati wa watu waliokuja kuwajulia hali ndugu zao.

Akizungumza hospitalini hapo Mkuu wa mkoa wa Mbeya  Bw.Kandoro aliwapa pole majeruhi na kuwataka wananchi kujitokeza kuchangia damu katika ajali hiyo ambapo alisema serikali imepeleka dawa na madaktari kusaidia kuwatibu majeruhi.

Pia amemtaka mwekezaji kusaidia chakula kwa majeruhi waliolazwa katika hopitali hiyo kutokana na kwamba asilimia kubwa ya majeruhi waliolazwa hapo ni wakazi wa nje ya eneo hilo.

Aidha ilidaiwa kuwa Lori hilo lilikuwa na abiria zaidi ya 200 ambao walikuwa na kawaida ya kupelekwa katika mashamba ya mwekezaji wa Kapunga na kurejeshwa jioni.

Post a Comment