Ads (728x90)

 



Add c
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kuanzia sasa hakitakubali kuwapokea mamluki kutoka CCM ambao hutumwa kwa ajili ya kukivuruga chama hicho.
Kauli hiyo imetolewa leo mchana na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na wanachama na wajumbe wa chama hicho kwenye uzinduzi wa Baraza la Uongozi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Bw. Mbowe amesema kuwa kundi la mamluki wanaotumwa kwa ajili ya kuvuruga upinzani halina nafasi ndani ya chama hicho kwa sasa na kwamba chama hicho hakitaendelea kuwavumilia wala kuwapokea mamluki hao.
Amesema kuwa CHADEMA haitapokea tena mamluki na kutoa onyo kwa viongozi waliopo ndani ya chama hicho kutotanguliza maslahi yao binafsi  badala ya maslahi ya nchi.Amesema migogoro mingi ya kisiasa ndani ya vyama vya upinzani inasababishwa na kupandikiziwa wanachama wasio waaminifu na waadilifu ambao nia yao ni kuvitengenezea migogoro vyama vyote vinavyokubalika na wananchi.
Amesisitiza kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Chama Taifa hatokubali kuiona hali hiyo kwa kuwa gharama ya kurejesha heshima ya chama inaweza kuchukua hadi miaka 20.Alitolea mfano vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF ambavyo vilikuwa na nguvu kubwa na kwamba vyama hivyo kwa sasa vimekosa mvuto kwa wananchi hali ambayo itavichukua muda mrefu kurejesha heshima yake.


aption





Post a Comment