Ads (728x90)





MFANYABIASHARA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Mfanyabiashara mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la Cosmas Kunzugala(60) ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Iyela Jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Diwani Athumani alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa na na watu hao majira ya saa 5:40 usiku.

Kamanda Diwani amesema kuwa mbinu iliyotumiwa na wauaji hao ni kumgongea mlango mfanyabiashara huyo ambapo mara alipotoka kufungua mlango alipigwa risasi kifuani na mkono wa kushoto na kufa papo hapo.

Amesema kuwa mara baada ya mauaji hayo wauaji hao walitokomea kusikojulikana ambapo hata hivyo alisema kuwa hakuna mali yoyote iliyochukuliwa ambapo mara baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuingia ndani.

Aidha Kamanda Diwani amesema kuwa katika eneo la tukio iliokotwa goroli moja ambayo hutumika katika bunduki aina ya Shirt Gun ambapo jeshi la polisi linachunguza   chanzo cha mauaji hayo na mwili wa marehemu umehofadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI

Post a Comment