Bloga Wetu Dodoma
ZIKIWA zimebaki dakika
345,600 sawa na saa 5,760 ambazo ni takribani siku 240 Rais Jakaya Kikwete
jana amefanya mabadiliko mengine ya Wakuu wa wilaya kwa kuwatupa nje ya ulingo wakuu
wa Wilaya 12 na kuteua sura mpya 27.
Uteuzi huo wa Rais Kikwete
umekuja huku kukiwa na tetesi za baadhi ya wakuu wa wilaya waliotemwa kupangiwa
kazi nyingine ikiwemo kuimarisha chama kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia
kufanyika Oktoba mwaka huu.
‘’Hakukuwa na sababu ya
kujiingiza gharama za kulipa wakuu wa wilaya watakaostaafu na kuachishwa kazi,
wakati tunakabiliwa na jukumu kubwa la zoezi la uandikishaji vitambulisho vya
kupigia kura na maandalizi mengine ya uchaguzi,JK alipaswa kuwaonea huruma
wananchi wake,’’alisema mkazi wa mjini Dodoma aliyejitambulisha kwa jina moja
la Mazengo.
Mazengo alisema kuwa kitendo hicho ni kuiingiza serikali gharama mpya ambayo haikupaswa kutokana na vipaumbele vilivyopo kwa mwaka huu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.
''Mahitaji yetu si kuwa na sura mpya za wakuu wa wilaya.. kimantiki hawa wapo kisiasa zaidi badala ya utendaji, wangebadilishwa watendaji huenda tungepata ladha ya kuwepo kwa mabadiliko haya,kwanini mabadiliko yafanyike ikiwa imebaki miezi nane JK amalize awamu yake? alihoji Mazengo ambaye kitaaluma anadai ni Mwalimu.
Katika uteuzi huo wa Rais
ambao umefanywa kwa niaba yake na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, JK amewapiga chini
wakuu wa wilaya 12 kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa ni umri, afya na kuimarisha
utendaji wa kazi serikalini.
Waziri Pinda aliwataja waliotenguliwa kuwa ni pamoja na James
Millya aliyekuwa Mkuu we wilaya ya Longido,Elias Lali aliyekuwa mkuu wa wilaya
ya Ngorongoro,Alfred Msovella aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kongwa ,Danny Makanga
aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kasulu,Fatma Kimario aliyekuwa mkuu wa wilaya ya
Kisarawe.
Wengine waliotenguliwa
ni Evarist Kalalu aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Mufindi,Abihudi Saideya
aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Momba Elibariki Kingu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya
Igunga,Dk.Leticia Warioba aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Iringa Martha Umbulla
aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kiteto,Khalid Mandia aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya
Babati na Elias Goroi.
Katika uteuzi huo wakuu wa
wilaya 27 wameula ambao ni pamoja na Mtangazaji maarufu wa TBC Shaaban Kissu,(Kondoa)Mariam
Mtima (Ruangwa),Dk.Jasmine Tiisike (Mpwapwa),Pololeti Mgema
(Nachingwea),Fadhili Nkurlu (Misenyi),Felix Lyaniva (Rorya),Fredrick
Mwakalebela (Wanging'ombe) na Zainabu Mbussi (Rungwe) .
Francis
Mwonga(Bahi),Kiming'ombe Nzoka (Kiteto),Husna Msangi (Handeni),Emmanuel Uhaula
(Tandahimba),Mboni Mhita (Mufindi),Hashim Mgandilwa (Ngorongoro) ,Mariam
Juma (Lushoto),Thea Ntara (Kyela) na Ahmad Nammohe (Mbozi)
Wengine ni aliyewahi kuwa
Kamanda wa Polisi katika baadhi ya mikoa hapa nchini Zelothe Steven
(Musoma),Pili Moshi (Kwimba),Mahmoud Kambona (Simanjiro) ,Glorius Luoga
(Tarime),Zainabu Telack (Sengerema),Benard Nduta (Masasi),Zuhura Ally (Uyui)
,Paul Makonda (Kinondoni),Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na Maftah Mohamed
(Serengeti).
Aidha Waziri Pinda
aliwataja wakuu wa wilaya 64 waliobadilishwa vituo vyao vya kazi kuwa ni pamoja na Nyerembe Munasa (Arumeru hadi Mbeya),
Jordan Rugimbana (Kinondoni hadi Morogoro), Fatma Salum Ally kutoka (Chamwino hadi
Mtwara), Lephy Gembe(Dodoma hadi Kilombero) na Christopher Kangoye (Mpwapwa
hadi Arusha).
Wengine ni Omar
Kwaang’(Kondoa- Karatu), Francis Mtinga (Chemba-Muleba), Elizabeth Mkwasa (Bahi-Dodoma),
Agnes Hokororo (Ruangwa –Namtumbo), Regina Chonjo kutoka (Nachingwea hadi Pangani),
Husna Mwilima (Mbogwe- Arumeru na Gerald Guninita (Kilolo – Kasulu).
Wengine waliobadilishwa
vituo vya kazi ni Zipora Pangani (Bukoba
hadi Igunga), Kanali Issa Njiku (Misenyi
hadi Mlele), Richard Mbeho (Biharamuro hadi Momba), Lembris Kipuyo (Muleba hadi
Rombo), Ramadhani Maneno (Kigoma kwenda
Chemba), Venance Mwamoto (Kibondo kwenda Kaliua), Gishuli Charles (Buhigwe
kwenda Ikungi), Novatus Makunga (Hai kwenda Moshi) na Anatory Choya kutoka (Mbulu
kwenda Ludewa).
Wengine ni Christine Mndeme
(Hanang’ kwenda Ulanga), Jackson Msome (Musoma kwenda Bukoba, John Henjewele (Tarime
kwenda Kilosa), Dk Norman Sigalla (Mbeya kwenda Songea), Dk Michael Kadeghe(Mbozi
kwenda Mbulu), Cripin Meela (Rungwe kwenda Babati) na Magreth Malenga (Kyela
kwenda Nyasa).
Aliwataja wengine kuwa ni
Said Amanzi (Morogoro kwenda Singida),Antony
Mtaka (Mvomero kwenda Hai), Elias Tarimo (Kilosa kwenda Biharamulo), Francis
Miti(Ulanga kwenda Hanang), Hassan Masala(Kilombero kwenda Kibondo),
Angelina Mabula (Butiama kwenda Iringa), Farida Mgomi (Masasi kwenda Chamwino),
Wilman Ndile (Mtwara kwenda Kalambo).
Pia aliwataja Ponsian Nyami
(Tandahimba kwenda Bariadi),Mariam Lugaila (Misungwi kwenda Mbogwe), Mary
Onesmo (Ukerewe kwenda Buhigwe), Karen Yunus (Sengerema kwenda Magu), Josephine Matiro (Makete kwenda Shinyanga), Joseph Mkirikiti (Songea
kwenda Ukerewe), Abdula Lutavi (Namtumbo
kwenda Tanga), Ernest Kahindi (Nyasa kwenda Longido), Anna Nyamubi (Shinyanga kwenda Butiama) na Rosemary
Kirigini (Meatu kwenda Maswa).
Abdalla Ali Kihato (Maswa
kwenda Mkuranga), Erasto Sima (Bariadi kwenda Meatu), Queen Mulozi(Singida
kwenda Ulambo), Yahaya Nawanda kutoka Iramba kwenda Lindi, Manju Msambya (Ikungi
kwenda Ilemela), Xaveli Maketta (Kaliua
kwenda Kigoma), Bituni Msangi (Nzega kwenda Kongwa) na Lucy Mayenga kutoka Uyui
kwenda Iramba.
Majid Mwanga amebadilishwa
kituo chake kutoka (Lushoto kwenda Bagamoyo), Muhingo Rweyemamu (Handeni kwenda
Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani kwenda Korogwe), Dk Nassor Ali Hamid (Lindi
kwenda Mafia), Festo Kiswaga(Nanyumbu kwenda Mvomero), Sauda Mtondoo(Mafia
kwenda Nanyumbu), Seleman Mzee (Kwimba kwenda Kilolo), Esterina Kilasi (Wanging’ombe
kwenda Muheza), Subira Mgalu(Muheza kwenda Karagwe) na Jacqueline Liana (Magu
kwenda Nzega).
Pia aliwataja wakuu wa
wilaya 42 waliobakishwa kwenye vituo vyao vya kazi kuwa ni Jowika Kasunga
(Monduli), Raymond Mushi (Ilala), Sophia Mjema (Temeke), Amani Mwenegoha
(Bukombe), Ibrahimu Marwa (Nywang’wale), Rodrick Mpogolo (Chato) Manzie
Mangochie (Geita), Darry Rwegasira (Karagwe), Luteni Kanali Bnedict Kitenga
(Kyerwa) na Constatine Kanyasu (Ngara).
Wengine ni Paza Mwamlima
(Mpanda), Peter Kiroya (Kakonko), Hadija Nyembo (Uvinza), Dk Charles Mlingwa
(Siha), Shaibu Ndemanga (Mwanga), Herman Kapufi (Same), Ephraimu Mbaga
(Liwale), Abdallah Ulega (Kilwa), Joshua Mirumbe (Bunda), Deodatus Kinawiro
(Chunya), Rosemary Senyamule (Ileje) na Galamhusein Shaban (Mbarali).
Wengine waliobaki ni
Christopher Mgala (Newala), Barika Konisaga (Nyamagana), Sara Dumba (Njombe),
Hanifa Karamagi (Gairo), Halima Kihemba (Kibaha), Nurdin Babu (Rufiji), Methew
Sedoyeka (Sumbawanga), Idd Kimanta (Nkasi), Chande Nalicho (Tunduru)), Senyi
Ngaga (Mbinga), Wilson Nkambaku (Kishapu) na Benson Mpesya (Kahama).
Wengine ni Paul Mzindakaya
(Busega), Georgina Bundala (Itilima), Fatma Toufiq (Manyoni), Luten Edward Ole
Lengai (Mkalama), Hanifa Selengu (Sikonge), Seleman Kumchaya (Tabora), Mboni
Mgaza (Mkinga na Seleman Liwowa (Kilindi).
Kwa mujibu wa Pinda
wakuu wa wilaya waliofariki ni Kapteni James Yamungu aliyekuwa mkuu
wa wilaya ya Serengeti,Anna Magoha aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Urambo na Moshi
Chang'a aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo.
Wakuu wa wilaya watano waliopandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa ni John Mongela aliyekuwa mkuu wa wilaya
ya Arusha amekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Amina Masenza aliyekuwa Mkuu wa wilaya
ya Ilemela amekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa,Dk.Ibrahim Khamis aliyekuwa Mkuu wa
wilaya ya Moshi amekuwa mkuu wa mkoa wa Katavi ,Halima Dendego aliyekuwa
mkuu wa wilaya ya Tanga amekuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara na Daud Ntibenda
aliyekuwa mkuu wa wilaya amekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.
Waziri Mkuu Pinda amewataka
wakuu wa wilaya waliobadilishwa vituo kuanza kazi mara moja huku ambapo wakuu
wa wilaya ambao wanaanza kazi hiyo kwa mara kwa kwanza wakisubiri kupatiwa
mafunzo ili kuboresha uwajibikaji wao.
Post a Comment