Ads (728x90)

 


 
 TIMU ya Prison ya Mbeya imeendelea kuutumia vibaya uwanja wake wa nyumbani kwa kulazimisha sare ya Bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani.
Ruvu ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Prison mnamo dakika ya 14 ya mchezo baada ya mchezaji aliyevalia jezi nambari 39 mgongoni Yahya Tumbo  kuwatoka walinzi wa Prison na kufunga bao kwa  njia ya Tik Tak.
Prison ambao walionesha kucheza chini ya kiwango walishambuliwa katika dakika za mwanzo huku wachezaji wake wakionekana kutoelewana vyema.
Hata hivyo katika dakika ya 30 ya mchezo wachezaji wa Prison walionekana kuamka na kulishambulia lango la Ruvu ambapo mchezaji Jacob Mwaitalako aliyeingia kipindi cha pili akawainua mashabiki kwa kusawazisha bao hilo.
Hadi mampumziko timu zote zilitoka kwa bao kufungana bao 1-1.
Kipindi chja pili hakikuzaa matunda kwa kila timu ambapo timu zote zilionekana kupaniana huku Prison iliyokuwa ikielekeza mashambulizi upande wa Kaskazini kukosa magoli mengi ya wazi.
Hadi kipyenga kinapulizwa Prison 1- Ruvu Shooting 1.

Post a Comment