Ads (728x90)

Golikipa wa Stend United John Mwenda akiuangalia mpira ukiwa umetinga wavuni baada ya mchezaji wa Prison Laurian Mpalile kuukwamisha mpira kimiani, huku wachezaji wengine Peter Mutabuzi(25) na Reyna Mgungira wakijaribu kuuokoa mpira huo

Kikosi cha timu ya Stendi ambacho kilichuana na timu ya Prison na kufungwa mabao 3-0

Benchi la Prison likiwa na baadhi ya wachezaji wa akiba wa timu hiyob
Kocha wa Prison Mbwana Makata akizungumzia hali ya mchezo baada ya kumalizika kwa 

NI magoli 3-0 ya timu ya Tanzania Prison ya Jijini Mbeya inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini dhidi ya Wapiga Debe wa Shinyanga Stand Unite, yameisaidia timu hiyo angalau kuwa na matumaini ya kuendelea kubaki katika Ligi Kuu iwapo wataendelea na ushindi kwa mechi zilizosalia.
Hata hivyo ushindi huo wa kimbunga dhidi ya timu ngeni katika ligi hiyo Stand bado unaibakisha timu hiyo katika nafasi ya mkiani ikiwa imejitwalia juma point 16 dhidi ya point 13 ilizokuwa nazo awali.
Ushindi huo wa Prison umetoa tafsiri halisi ya maamuzi magumu yaliyofanywa na timu hiyo ya kumtema aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo David Mwamwaja na mikoba yake kurithiwa na Mbwana Makata ambaye amewakiwa na nyota njema ya ushindi wa kimbunga.
Ushindi wa Prison ulianza kuonekana dakika za mwanzo za mchezo huo ambapo vijana hao tofauti na ilivyokuwa katika michezo mingine walionekana kujituma na kucheza kwa ari kubwa ya kuhitaji ushindi.
Wasambuliaji wa Prison akina Jeremia Juma Jimmy Shoji,Amir Omar na Hamisi Maingo walionekana ni mwiba mchungu kwa walinzi wa Stendi akina Abuu Ubwa, Jisendi Maganda,Peter Mutabuzi na Reyna Mgungira.
Golikipa wa timu ya Stend John Mwenda alikuwa na kibarua kizito cha mashambulizi kutoka kwa washambuliaji wa Prison ambao walionekana kucheza bila kuchoka kutoka mwanzo mwa mchezo hadi mwisho.
Mashambulizi hayo ya mara kwa mara katika goli la Stendi yalizaa matunda katika dakika 30 ya mchezo ambapo Beki wa Prison Laurian Mpalile alipoipatia timu yake bao la kwanza baada ya kuwatoka walinzi wa Stendi na kumimina shuti kali lililomwacha golikipa wa Stendi John Mwenda akichupa bila mafanikio.
Goli hilo liliamsha hamasa kwa wachezaji wa Prison na kucheza kwa kuonana vyema huku wachezaji wa Stendi ambao wanaonekana kama bado hawajaizoea mikiki mikiki ya ligi hii wakipigiana pasi mbovu na mipira kuwafikia wachezaji wa Prison.
Hata hivyo almanusura mashabiki wa timu hiyo kongwe katika ligi hiyo waingie nyongo kwa kujifunga wenyewe baada ya mchezaji wake Salum Kimenya kupiga tiktaka iliyokatwa na upepo na kuelekea golini kwake ambapo hata hivyo golikipa Mohamed Yusuf wa  Prison alipangua mpira huo uliopita juu ya mwamba na kusababisha kona.
Mashambulizi ya uchu wa kupata magoli ya Prison yaliendelezwa kwa kasi kubwa na kusababisha dakika ya 41 Amir Omar kuwatoka walinzi wa Stend na kubaki na golikipa John Mwenda na kuukwamisha mpira nyavuni lakini mshika kibendera wa upande wa mashari ya uwanja alinyoosha kibendera cha kuotea kwa mchezaji huyo.
Hadi filimbi ya mapumziko inapulizwa Prison walitoka kifua mbele kwa goli 1 -0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa kwa wachezaji wa Prison kuonesha kandanda safi huku wachezaji wa Stend wakihaha kusawazisha bao bila mafanikio.
Ilikuwa ni timu ya Prison tena mnamo dakika ya 52 ya mchezo ambapo mara hii mchezaji Hamisi Maingo aliwainua mashabiki wa timu hiyo kwenye viti kwa kushangilia baada ya kuopachika bao maridadi lililotokana na pasi ya mshambuliaji mrefu Ibrahimu Is- haka.
Maingo mara baada ya kupokea pasi kutoka kwa Is haka aliwalamba chenga walinzi wa Stend Jisendi Maganda,Abuu Ubwa na Peter Mutabuzi na baadaye kumlamba chenga golikipa na kutingisha wavu na kulifanya ni goli la 2 kwa Prison.
Kama vile haikutarajiwa mashabiki waliozoeleka kutoishangilia timu ya Prison ambao mara nyingi huketi katika jukwaa la kaskazini waliinuka vitini na kushangilia goli hilo na hivyo kurejesha uhai kutokana na uhasama mkubwa uliopo baina yao wanafamilia wa timu hizo mbili.
Bao hilo lilizidi kuwachanganya wachezaji wa timu ya Stendi United yenye kawaida ya kuwa na mashabiki wenye vurugu kubwa uwanjani wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani na hivyo kuonekana kama walionywea na kuloa maji ya baridi.
Kuchanganyikiwa kwa wachezaji hao kuliendelea kuamsha ari kwa wachezaji wa Prison ambao walilishambulia goli la United kama nyuki na kusababisha msukosuko katika lango lao na hivyo kusababisha kona katika dakika ya 60.
Kona hiyo iliyochongwa kiufundi na  Jeremiah Juma ilitua katika kichwa cha Hamis Maingo ambaye bila ajizi aliruka kama Nyani na kupiga m;pira huo kwa kichwa na mpira kutinga wavuni na kumwacha golikipa na walinzi wa Stend wakishindwa kuamini macho yao.
Baada ya kuingia kwa goli hilo wachezaji wa Shinyanga walionekana kukata tamaa huku wakiwa wamechoka kupita kiasi ilhali wenzao wa Prison wakizidi kuongeza kasi wakihitaji kuongeza bao la 4.
Hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa Prison walikuwa kifua mbele kwa goli 3 didi ya 0 ya Stendi United.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha mpya wa Prison Mbwana Makata alisema kuwa, amejitahidi kuwatyuni kisaikolojia wachezaji wake na kuwajengea uwezo mpya katika kukabiliana na janga la kushuka daraja kwa timu yao.
Kwa upande wake Kocha wa United Mathias Lule mbali na kukubali kushindwa katika mchezo huo alitupia lawama waamuzi(bila kufafanua zaidi) kwamba walikuwa wakichezesha mpira kwa upendeleo.

Timu ya Stendi inaelezwa itaendelea kubaki Jijini Mbeya ikisubiri mechi yake Mbeya City inayitarajiwa kupigwa katika dimba hilo Jumatano ijayo, huku Mbeya City wakiwa wanatarajia kukabiliwa na kibarua kigumu katika mchezo wake kesho atakapokumbana na Maafande wa Tanga Mgambo Shooting.

Post a Comment

  1. We From SEO Milanisti Introduces Its Sales Sells Herbal Products Men And Women ALL PRODUCTS FROM our clients in Down's.

    pembesar penis | obat pembesar penis

    parfum pemikat wanita | perangsang wanita

    ReplyDelete