Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa wanaosubiri huduma kwenye hospitali ya wazazi Meta Jijini Mbeya leo asubuhi |
Makalla
ametoa siku 7 kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya wazazi ambayo iko chini ya
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo ameunda tume ya watu wanne akiwemo
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo kuchukua
kufanya uchunguzi na kuchukua hatua.
Tume ya watu
wanne iliyoundwa kufuatilia tuhuma hizo inamhusisha Mkurugenzi wa Hospitali
hiyo, Matroni, Patroni na Mjumbe mmoja kutoka Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya.
Makalla
alisema lengo la kuundwa kwa tume hiyo ni kwa ajili ya kupata ukweli juu ya
kutolewa kwa lugha chafu kwa mgonjwa huyo ikiwa ni pamoja na kupata upande wa
pili wa Muuguzi aliyetuhumiwa ambaye hakuwepo hospitalini hapo wakati wa ziara
yake.
Sanjari na
tukio hilo Mheshimiwa Makalla amekutana na kero ya msongamano wa wagonjwa
mawodini hali ambayo imesababisha baadhi ya wagonjwa kukosa vitanda na wengine
kulala kitanda kimoja zaidi ya mtu mmoja.
‘’Nawaomba
madaktari na wauguzi, fanyeni kazi kwa kuzingatia maadili wakati mnapotekeleza
majukumu yenu.
Aidha Mheshimiwa Makalla amesema kuwa atafuatilia wizara ya Afya ombi la ujenzi wa wodi ya wazazi ambayo ni dhamana ya mkopo kutoka hazina fedha ambazo hospitali hiyo iliomba hapo awali.
Aidha Mheshimiwa Makalla amesema kuwa atafuatilia wizara ya Afya ombi la ujenzi wa wodi ya wazazi ambayo ni dhamana ya mkopo kutoka hazina fedha ambazo hospitali hiyo iliomba hapo awali.
Post a Comment