Ads (728x90)


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya LAFARGE Ilse Boshoff akimkabidhi Meneja wa Mahusiano Allan Chonjo mfuko wa saruji aina ya Tembo Fundi mara baada ya uzinduzi ulifanyika kiwanda cha Saruji Songwe kilichopo Mkoani Mbeya juzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Lafarge Tanzania Ilse Boshoff akiwa pamoja na mameneja wa vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo mara baada ya uzinduzi wa saruji ya Tembo Fundi kwenye kiwanda cha Saruji cha Songwe mkoani Mbeya

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Saruji ya Lafarge akielezea faida na matumizi ya saruji mpya rafiki kwa mafundi waashi ya Tembo Fundi

Wasanii wa kikundi cha sarakasi wakionesha burudani wakati wa uzinduzi wa saruji ya Tembo Fundi Songwe mkoani Mbeya hivi karibuni





Kampuni ya Saruji Lafarge Tanzania imezindua saruji ya kwanza maalumu kwa matumizi ya uashi. Saruji hii inayojulikana kama Tembo Fundi itawapa wajenzi chaguo bora kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni pamoja na kupiga plasta ukuta, kusakafia, kujengea tofali na kupangilia marumaru.



Saruji hiyo iliyotengenezwa maalum kwa kazi ya uashi wa kuta za nje na ndani ina ubora katika kufanya kazi, nguvu kwenye ugundishaji inashika vizuri na ina umaliziaji bora wenye kuleta matokeo yaliyo

bora zaidi kwenye kujenga tofali, uzio, marumaru na sakafu.



Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Ilse Boshoff, alisema wakati wa uzinduzi leo kwamba Tembo Fundi imeundwa mahususi kwa ajili ya kazi za uashi na kuwapa wajenzi utendaji bora wa kazi na thamani ya fedha.



“Ikiwa imetengenezwa kutokana na uzoefu na utaalamu wa Lafarge kimataifa katika kuzalisha saruji, Tembo Fundi ni rahisi kutumia katika kupiga plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla ambayo itamchukua muashi muda mrefu katika kusawazisha ukuta.



Alisema faida nyingine muhimu katika matumizi ya Tembo Fundi ni unafuu katika gharama kutokana na mfuko mmoja wa Tembo Fundi kutumika eneo pana zaidi ukilinganisha na mfuko wa saruji ya matumizi ya jumla. Kutokana ya kwamba inafanya kazi vizuri na uimara wake kudumu kwa muda mrefu Tembo Fundi itawasaidia wajenzi kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.


LAFARGE TANZANIA
Mbeya Cement Co. Ltd | Oyster Plaza, 3rd Floor | Plot 1196 Haile Selassie Road
P.O. Box 46452 | Dar Es Salaam - Tanzania - ( office +255 222 923 300\1
Songwe Industrial Area | Tunduma Highway
P.O. Box 529| Mbeya – Tanzania ( office +255 252 950 005/6

Post a Comment