Ads (728x90)

Maisha ni kuhangaika maisha ni kutafuta hata watoto nao wanahangaika na maisha katika kipindi cha likizo wakitafuta fedha za kujikimu mara ifunguapo shule.

Mtoto huyu anaokekana akiwa na maparachichi  kichwani akitafuta wateja,huamka asubuhi na kuzunguka mjini hadi jioni ili angalau aweze kujipatia senti za kujisaidia.
Ni wakati wa msimu wa likizo watoto wengi hujishughulisha na biashara ndogondogo ili kuwasaidia wazazi wao kujikimu kimaisha akama wanavyoonekana baadhi ya watoto katika maeneo mbalimbali,mtoto huyu anaonekana akiuza mapapai, 
Naye mtoto huyu kama alivyo yule anayeuza mapapai anajikimu kwa kuuza ndizi mitaani kila siku ili hatimaye siku inapofunguliwa shule amudu kujinunulia madaftari.

Mtoto huyu naye hakuwa nyuma katika kujitafutia riziki alionekana akiuza mahindi mabichi mitaani.

Naye huyu alikutwa na mwanablog wetu akihaha mitaani akijitafutia riziki kwa kuuza maparachichi

Post a Comment