Ads (728x90)

Nineneje nijivune,uneni naye Makene,
Mtambaji wa karine,bloguni jivunia.

Makene ni mtambaji, bloguni jivunia,
Chakuvunia kipaji, fasihi ziso udhia.

Japo ningile kwa kasi, bali njia kupitia,
Ili nipate wepesi,bloguni tangazia.

Kubwa lilohitajia, kiswahili kukuzia,
Ulumbi si njema njia,fasihi kutangazia.

Mikono naashiria, kuiacha hii njia,
Hima chini kuketia, nudhumu kuitumia.

Nunu sineni Makene,kwa njia ya mapene,
Kwa lako hili sebene,wastahili jivune.

Wakatabahu uneni,sitarazii mengine,
Swahili tutumieni,kufunda waso uneni.

Post a Comment

  1. Nimesikia Mkwinda, nafunga wangu ugani
    Nimekuona kiwanda, kwa ghafi ulotunzani
    Najua waweza shinda, malenga kubakiani
    Mkwinda nafunga hoja, U mzima utembee.

    Majibizano ya gani, utamu yanaletani
    Hugeuka mtihani, malenga vina pangani
    Kisha hamu hujengani, mengi shairi tungani
    Mkwinda nafunga hoja, je kura umepigani?

    Mimi malenga wa bara, hilo basi tambuani
    Jina langu Nakuzerwa, shairini tambiani
    La kaka nilichukuwa, tangu alipopishani
    Diwani nikatungani, zasubiri chapishwani.

    Aliitwa Benjamin, Mwalimu asoudhia
    Hakutimu kipindini, Kansa ikambebani
    Mkwinda ninakwambiani, imani nimejengani
    Nafasi wachukuani, kaka mpya malengani!

    Kaka sasa fungulia, ulotimia ugani
    Utunge kuhaditrhia, ujio wao wageni
    Lugha wanachafulia, dhahabu sumu wekani
    Nakimbia darasani, mtihani kufanyia.

    ReplyDelete
  2. Nimesikia Mkwinda, nafunga wangu ugani
    Nimekuona kiwanda, kwa ghafi ulotunzani
    Najua waweza shinda, malenga kubakiani
    Mkwinda nafunga hoja, U mzima utembee.

    Majibizano ya gani, utamu yanaletani
    Hugeuka mtihani, malenga vina pangani
    Kisha hamu hujengani, mengi shairi tungani
    Mkwinda nafunga hoja, je kura umepigani?

    Mimi malenga wa bara, hilo basi tambuani
    Jina langu Nakuzerwa, shairini tambiani
    La kaka nilichukuwa, tangu alipopishani
    Diwani nikatungani, zasubiri chapishwani.

    Aliitwa Benjamin, Mwalimu alosheheni
    Hakutimu kipindini, Kansa ikambebani
    Mkwinda ninakwambiani, imani nimejengani
    Nafasi wachukuani, kaka mpya malengani!

    Kaka sasa fungulia, ulotimia ugani
    Utunge kuhaditrhia, ujio wao wageni
    Lugha wanachafulia, dhahabu sumu wekani
    Nakimbia darasani, mtihani kufanyia.

    ReplyDelete
  3. tuso kauli
    wala ilihali
    mizani imegoma akilini.

    Yetuye macho!

    ReplyDelete