Ads (728x90)

Chachandu iliyochacha, si chachandu chachizi,
Huuchachuza mchicha,na kuchachiza mchuzi,
Huchuruza kwe'pakacha,churuzo ya uchirizi,
HUCHACHIZIA MCHUZI, CHACHANDU ILIYOCHACHA.

Chanchandu iliyokacha,hutaghayari churuzi,
Uonjapo utaacha,kwa kuchelea ushuzi,
Utashidna kutwa kucha,kwa kula viso ujuzi,
HUCHACHIZIA MCHUZI, CHACHANDU ILIYOCHACHA.

Chachandu iliyochacha, walao huziba tuzi,
Matumbo yao huchacha,kupenda vya upuuzi,
Tamathali ya machicha, chujo la tui na nazi,
HUCHACHIZIA MCHUZI,CHACHANDU ILIYOCHACHA.

Ja tunmgo za kuparacha,mithali iliyowazi,
Nyembo usiwe picha, fashi ni nzito kazi,
utaparua makucha, na kutunga ubazazi,
HUCHACHIZIA MCHUZI,CHACHANDU ILIYOCHACHA.

Tungo zawa parakacha,zaonekana wazi,
Iwapo tutaziacha zitadodesha utunzi,
Si tungo bora kuacha, sije leta uchafuzi,
HUCHACHIZIA MCHUZI, CHACHANDU ILIYOCHACHA.

Tamati beti nazicha, Nyembo takupiga konzi,
Nalonga pasi kuficha, U kinda kwa hii kazi,
Ushairi utakacha, ujeranda kama chizi,
HUCHACHIZIA MCHUZI, CHACHANDU ILIYOCHACHA.

TUNGO HII NI CHANGAMOTO KWA MALENGA WAPYA, ILI KUJARIBU KUBORESHA KAZI ZAO HUSUSAN Bw. Nyembo wala usijisikie vibaya umekuja vizuri naomba uje na kitu kipya ili angalau tumuunge mkono, Makene, Mwandani na wengineo tutumiao ushairi katika blogu hii.

Haya shime Nyembo kaza buti umenichangamsha sana kwa shairi lako la kujibu TA, TE, TI, TO, TU.

WAKATABAHU

Post a Comment

  1. Mkwinda sijibu kwa shairi sasa lakini nimecheka sana hapa. Haya kazi kwako Nyembo nangoja ushuke mistari kisha nami nikuongezee nguvu.

    ReplyDelete
  2. bismilah naanza,kwa jina lako muweza,
    Bloguni kushangaza,na Rashidi aso weza,
    huyo ananishangaza,katika hili baraza,
    yupo aliyechachaza,mchuzi safi kuchacha.

    Mkwinda umechachaza,sasa sauti kupaza,
    Harufu umesambaza,ukinywa bila kusaza,
    taarifa natangaza,kukujibu ninaweza,
    yupo aliyechachaza,mchuzi safi kuchacha.

    Naam,nimekosa muda tu kaka,lakini ningejibu ili kuongeza ujuzi ingawa hii fani ni ngumu,nami si mjuzi lakini kadiri ya hali nitajitahidi,kwani nyie mlizaliwa mnatunga? tena moto huanza cheche..pokea basi cheche uzibariki ziwe moto.

    ReplyDelete
  3. Kumbe wazijua nyimbo, vipi unaweka giza,nimeona zako tambo,'ngawa nimekuchakaza.
    Waweza pita mgambo, kwa mshipa kuukaza,Sasa nakupa majambo, tunga pasi kucharaza.

    Tunga sasa Bw.Nyembo, Hiyo ndo njia ya kwanza,utakutana na tambo, zitambazo kwenye chaza,Medani zikawa lumbo, nawe ushindwe kuweza.

    Tunga usipigwe kumbo,huu uga kutopaza,Bali tunga kwa vina kupanga nimekutunuku mikoba.

    WAKATABAHU

    ReplyDelete
  4. Unajua Makene huyu Yakub nimemchangamsha ili ajue kuwa kwamba kuna baadhi ya watunzi wa ushairi ni vichaa, hivyo nimemkaribisha kwa tambo hizo ili ajue namna ya kupambana na walumbaji mahiri....tunaweza kulumbana basi tu, enzi zile katika gazeti la Uhuru na Mzalendo tulikuwa na akina Said Nyoka(Udogo si hoja)Jumaa Mgwadu( Sheikh wa Mkoa)Marehemu Said Mgwalla,Abdallah Matawa,Adidi Rugemarila,Ally Hengo na wengine wengi tulichangamsha sana uga wa malenga tukiongozwa na Mzee wetu Amir Sudi Andanenga(Sauti ya Kiza) sasa kasi ile tukiingiza katika Blogu nakwambia patakuwa hapatoshi!!!!! we! acha tu.

    ReplyDelete
  5. Nafurahi sana kuona uga wa malenga unahamia kwenye blogu. Tulizoea kusoma kwenye gazeti la uhuru. Sasa tunazuuzika kukutana na vichaa wa aya kwenye mtandao pepe.

    ReplyDelete
  6. mimi naona niwaombe radhi wasomaji wako Bw. Mkwinda,mjadala huu nami naupandisha katika Blog yangu kwa kuwa sijaridhika kwa uliyomwambia Makene hivyo napanda kwanza kwa swali kama kukueleza jambo hakufai kwanuka kama chachandu na mchuzi ulo chacha,basi nikome kusema yanayohusiana nawe....

    ReplyDelete
  7. @Nyembo,
    Umeniacha hoi uliposema "kwani nyie mlizaliwa mnatunga? tena moto huanza cheche pokea basi cheche uzibariki ziwe moto....

    Kazi anayo bwana Mkwinda.

    ReplyDelete
  8. mkwinda!

    tuliishakuomba! anzisha archive (makumbusho) ya mashairi yoooote yaliyokuwa kwenye uhuru na mzalendo tangia mwanzi wa hayo magazeti uingize kwa intaneti kama archives. nimeishawahi kufanya sanaa. ninachojua ni kwamba utunzi hutegemea mambo mengi na haswa wakati uliopo. mtu utajitahidi sana lakini hutaweza kupata mguso wa shairi lililotungwa wakati ule. mfano sasa hivi mtu huwezi ukatunga shairi kuhusu utamu wa mabungo au umuhimu wa yale matunda alita - kama sabuni!!mashairi ya sasa yanaakisi mabadiliko na tekenologia. yake ya wale wazee yanagusa zaidi mambo ya porini porini na uhusiano wa mtu na asili zaidi na ndio kwa kupatia amani. itahuisha pia asili ya mwanadamu kwa kizazi hiki na kijacho!!lakini najua gharama yake, ni mradi mkubwa - hata hivyo hii wizara ya utamaduni inapaswa iunge mkono hili wazo. - tupo kuunga mkono bidii hii!

    ReplyDelete
  9. Nashukuru Bw. Msaki nitajitahidi kufanya hivyo ingawa itakuwa kazi kupata nakala za magazeti zile za zamani ila nitajaribu kutafua yale mashairi yangu ya enzi zile niyaingize katika Blogu wasomaji wetu wanufaike wapate kumbukizi zile zilizotamba na kuwafanya hata wahariri wasitishe baadhi ya malumbano ambayo yalikuwa yakielekea kuliko siko

    ReplyDelete
  10. Hakika nimegundua, tamu yazaa kichaa
    Uchungu napandishia, Nyembo hapa msemea
    Mistari kapashia, ujumbe kutuwachia
    Sasa tunatamkia, Malenga ajipe jina!

    ReplyDelete
  11. jina langu hudhud,kwa sifa za maabudi,
    zuri kama uwa ridi,kwa tungo za al-ud,
    shukrani kwa wadudi,kunipa hizi bidii,
    sasa nakutamkia,malenga najipa jina.

    Mh! KWA KWELI NAFURAHI SANA KUONA USHIRIKI WETU KATIKA TAMBO HIZI,NI NJIA YA KUONGEZA MSAMIATI WA LUGHA ADHIMU YA KISWAHILI

    ReplyDelete
  12. mkwinda, anza na yako, lakini pia niachojua ukienda katika maktaba za taifa mikoa na vyuo hata kwa uhuru wenyewe magazeti yoote wanayo..utashangaa sana...uhuru pia wanayo maktaba yao kwa ajili ya hili...labda unapoanza pia tuandikia uliliandika lini ulikuwa unafikiria nini na tarehe lililotoka gazetini na gazeti gani...

    najua kufanya kazi kubwa kama hii inabidi uache kila unachofanya ili ubuni sio tu kuendelea kubandika bloguni ila bustani ya washairi kama page ya internet.

    ni vyema zaidi shughuli hii ukairasmisha. yaani hata wewe sasa uache kibarua chako cha sasa uhamie kwenye ofisi hii mpya...nyembo aweza kukusaidia...na mimi niko tayari kwa hilo...

    ni juhudi...na mambo ya kufanya kwa kila mmoja wetu ni mengi sana duniani. tumemuona teyari ndesanjuo anafanya juhudi zake...kwa anga zake za utaalamu..wanapambana na hatimiliki kwa mabo yote...ni ukombozi kwa namna fulani...wewe na nyembo munaweza kuanzisha hili....na ninaamini kabisa wizara ya utamaduni / wafadhili inaweza kufadhili hii shughuli...

    ni muhimu sana ili urithi wa taifa usife....ina maana magazeti yoote yakiungua na wote wa kizazi hiki tukafa ndio mwisho wa fasihi hii zama za awali ambazo ni muhimu kutengeneza mrejesho nyuma wa fasihi yetu...cha ajabu sana marekani wametunza mashairi yao tangu mwanzo wa taifa lao...mengine hadi juzi kina tupac - "makaveli" walikuwa wanayaimba..niligundua hii pale nation library dar nikipitia fasihi za marekani...

    ReplyDelete
  13. mkinda jambo jengine rahisi ni kuwasiliana na hao watunzi woote wenzio wa zama hizo wakupe madaftari yao nina uhakika wameyatunza, lini waliandika, na yalitoka gazeti gani...huo ni ushindi mkubwa kitachobaki ni kujazia jazia na kutafuta secretary wa kuchapa tu basi!!

    ReplyDelete
  14. samahani kurudirudi, nadhani ni rahisi mkiwa na scanner, ukipata hizo kurasa za magazeti unascan kama text ambazo ni editable....kisha unazisevu upya si unanipata? watu kama kina michuzi ni muhimu sana kushirikishwa kwenye huu mradi kwani wana access na archive za chamana serekali..si unaona hizo picha anazotuwekea?

    ReplyDelete
  15. Asante Msaki kwa ushauri wakao nitajaribu kuwashirikisha washairi wengine juu ya hili Nyembo nadhani kishalipata hili kazi kwetu

    ReplyDelete