Ads (728x90)

Wadau wa elimu wakitoka kuangalia eneo la ujenzi wa shule kijiji cha manga wakiongongozwa na  na kaimu mkurugenzi mtendaji wilaya ya Mpanda.
Mkuu  wa wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga akielezea jambo kuonesha alivyokubali ushirikiano wa wadau wa maendeleo katika wilaya yake kwa kuwawezesha vijana kuboleshea miundombinu ya maji  na kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha vijana kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya mlele Kanal Ngemela Lubinga na Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Mpanda na Mlele MwlNaomi Nnko wakibadilishana jambo  muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na wadau wa maendeleo ofisini kwake.
Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Mpanda na Mlele akisaini kitabu cha wageni katika kijiji cha manga muda mfupi alipoembela kijiji hicho akiwa na wadau wa maendeleo wanaotarajia kujenga shule ya sekondari ili kuboresha utoaji wa taaluma na kusogeza maendeleo karibu ya kielimu katika kijiji hicho.
.Kaimu Afisa mipango wa Wlaya ya Mpanda Paul Ibrahimu Kahoya akiwa ofisi akiratibu shughuli mbalimbali za maendeleo katika wilaya yake,ofisi ya mipango ndiyo inayoratibu shughuli zote za maendeleo katika wilaya na kila mradi kabla ya kutekelezwa lazima upitie ofisi ya mipango ambapo wachumi huwa wanabanga na kuratibu kwa maana nyingine twaweza sema injini ya maendeleo katika halamashauri.
(Picha zote na Kibada Kibada.- Mpanda Katavi)



Post a Comment