Ads (728x90)

Kocha msaidizi wa kikosi cha maboresho cha Taifa Stas Salum Mayanga akizungumza na waandishi wa habari uteuzi wa wachezaji 16 kati ya wachezaji 34 waliokuwa katika kambi ya Tukuyu wilayani Rungwe kwa wiki tatu.
 
 
Chama cha Mpira wa miguu nchini (TFF) kimetaja majina ya kikosi cha wachezaji 16 kwa ajili ya  maboresho ya timu ya Taifa Stars kati ya wachezaji 34 waliokuwa katika kambi ya wiki tatu mjini Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Kikosi hicho ambacho kimeelezwa kuwa ni cha maboresho kinatarajia kucheza mechi mbalimbali za kirafiki ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hotel ya Hill View Jijini Mbeya kocha msaidizi wa kikosi hicho Salum Mayanga alisema kuwa wachezaji walioteuliwa ni pamoja na Mlinda mlango Benedict Tinoko(Mara),Walinzi wa kati Emma Namwondo Simwanda(Temeke)Joram Nason Mgeveje(Iringa).

Aliwataja walinzi wa pembeni  kuwa ni Omar Ally Kindamba(Temeke)Edward Peter Mayunga(Kaskazini Pemba),Shirazi Abdallah Sozigwa(Ilala) na viungo wa ulinzi ni Yusuf Suleiman Mlipili(Temeke) na Said Juma Ally(Mjini Magharibi).

Wengine ni viungo wa ushambuliaji Abubakar Ally Mohamed(Kusini Unguja)Hashimu Ramadhan Magona(Shinyanga) ambapo viungo wa pembeni ni Omar Athuman Nyenje(Mtwara), Chunga Said Zito(Manyara) na washambuliaji wanne ambao ni Mohamed Seif Said(Kusini Pemba)Ayubu Kassim Lipati(Ilala) Abdulrahman Othman Ally(Mjini Unguja) na Paul Michael Bundala(Ilala).

Pia Kocha Mayanga aliwataja wachezaji wawili wa U-20 watakaojiunga na timu Serengeti Boys kuwa ni Mbwana Mshindo Mussa kutoka mjini Tanga na Bayaga Athanas Fabian kutoka mkoani Mbeya.

Hata hivyo alisema kuwa wachezaji 16 waliobaki wataendelea kuwa chini ya uangalizi kwa ajili ya kuziba mapengo kwa timu ya Taifa na kwamba mchakato wa uteuzi wa wachezaji hao ambao ni mpango mpya wa chama cha Mpira wa miguu nchini TFF kuimarisha kikosi cha timu ya Taifa umefanyika mara nne ambapo awali jumla ya wachezaji 143 walijitokeza na kuchujwa hadi kufikia idadi ya wachezaji 16.


Post a Comment