Ads (728x90)



MKUTANO WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NA VYOMBO VYA HABARI “PRESS CONFERENCE” TAREHE 18.04.2014.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi anatumia fursa hii kukutana na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari ikiwa ni nafasi ya kutoa tathmini ya Hali ya Uhalifu kwa Mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha robo – mwaka Jan-Machi, 2014, pia kusikia maoni, ushauri na changamoto mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari kwa lengo la kujenga na kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.


TATHIMINI YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA JAN-
      MACHI, 2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN- MACHI, 2013.

1.      TATHMINI YA MAKOSA YOTE YA JINAI.

Katika kipindi hicho cha Jan – Machi, 2014 jumla ya makosa 6,473 yaliripotiwa, wakati kipindi kama hicho mwezi Jan – Machi, 2013 makosa 6,853 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 380 sawa na asilimia 6.

2.      TATHMINI YA MAKOSA MAKUBWA YA JINAI.

Katika kipindi hicho cha Jan – Machi, 2014 jumla ya makosa makubwa 594 yaliripotiwa, wakati kipindi cha Jan-Machi, 2013 makosa 601 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 7  sawa na asilimia 1.

3.      TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO YA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU WENGINE.

 Aidha  katika kipindi cha  Jan –  Machi, 2014  makosa makubwa yatokanayo  na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali  katika kufanya doria,misako na operesheni katika kupambana na uhalifu na wahalifu  yaliripotiwa matukio  128, wakati kipindi cha  Jan- Machi, 2013 yaliripotiwa makosa 121,  hivyo kuna ongezeko la matukio 7, sawa na asilimia 84






4.      TATHMINI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.

§  Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa/matukio yote yaliyoripotiwa katika kipindi cha Jan – Machi, 2014 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji ni 12,250 wakati kipindi kama hicho Jan-Machi, 2013 yaliripotiwa makosa 14,375 hivyo kuna pungufu ya makosa 2,125 sawa na asilimia 15.

§  Matukio ya ajali yaliyoripotiwa kwa kipindi cha JanMachi, 2014 yalikuwa 98 wakati kipindi cha Jan- Machi, 2013 yalikuwa 156  hivyo kuna upungufu wa matukio 58 sawa na asilimia 37. Matukio ya ajali za vifo yaliyoripotiwa Jan – Machi,  2014 yalikuwa 58 wakati kipindi cha Jan-Machi, 2013  yaliripotiwa matukio 65  hivyo kuna pungufu ya matukio 7 sawa na asilimia 11.

§  Watu waliokufa kipindi cha Jan-Machi, 2014 walikuwa 61 wakati Jan –Machi, 2013 walikuwa 81 hivyo kuna pungufu ya watu 20, sawa na asilimia 7. Watu waliojeruhiwa kipindi cha Jan – Machi,   2014 walikuwa watu 104 wakati Jan – Machi, 2013 walikuwa watu 91 hivyo kuna ongezeko la watu 13,  sawa na asilimia 14.

§  Katika kipindi cha Jan – Machi, 2014,  jumla ya makosa 12,422  ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo la Tshs 332,790,000/=  ikilinganishwa na tozo la Tshs 365,400,000/=  iliyokusanywa katika kipindi Jan – Machi, 2013  kutokana na makosa 14,219, hivyo kuna pungufu la kiasi cha Tshs 32,610,000/=  sawa na asilimia 9.

5.  MAJEDWALI KUONYESHA HALI YA UHALIFU.

MCHANGANUO WA MAKOSA YOTE MAKUBWA YA   JINAI NA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI CHA FEB -   2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN - MACHI, 2013.


           MAKOSA
JAN–   MACHI 2014
JAN      MACHI   2013
TOFAUTI +/-
ASILIMIA %
                                                               
MAKOSA DHIDI YA BINADAMU
MAUAJI
53
82
-29
-35
KUBAKA
129
98
+31
+32
KULAWITI
14
5
+9
+180
KUTUPA MTOTO
2
5
-3
-60
USAFIRISHAJI BINADAMU
3
1
+2
+200
JUMLA
201
191
+5
+3


-          Mauaji - Wilaya iliyoongoza ni  Mbeya 13,Momba 10 na Chunya 9.
-          Kubaka- Wilaya iliyoongoza ni  Mbeya 60, Chunya 21 na Rungwe 14. 
-          Kulawiti – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 6 na Mbarali 2.
-          Usafirishaji wa binadamu – Wilaya iliyoongoza ni Mbozi 1/Momba 1 na Mbarali 1. 



  
                                                                     
MAKOSA DHIDI YA KUWANIA  MALI
UNYANG’ANYI WA K/SILAHA
3
4
-1
-25
UNYANG’ANYI WA K/NGUVU
25
46
-21
-46
UVUNJAJI
92
109
-17
-16
WIZI
873
989
-116
-12
WIZI WA PIKIPIKI
52
26
+26
+100
WIZI WA MIFUGO
59
59
-
-
JUMLA
1,104
1,233
                 -129
-10

-          Unyang’anyi ktk Barabara Kuu – Wilaya iliyoongoza ni Mbarali 1.
-          Unyang’anyi wa kutumia nguvu – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 8 na Momba 8/Chunya 8.
-          Uvunjaji - Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 22, Momba 18 na Kyela 13.
-          Wizi wa Pikipiki –Wilaya iliyoongoza ni Chunya 18, Mbeya 14 na   Kyela 8
-          Wizi wa Mifugo – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 10, Mbarali 3 na Chunya 2.
                                         
MAKOSA DHIDI YA MAADILI YA JAMII
[YATOKANAYO NA JITIHADA ZA POLISI  KWA USHIRIKIANO NA WADAU NA WANANCHI MBALIMBALI]
KUPATIKANA NA SILAHA
8
4
+4
                  +100
BHANGI
60
66
-6
-9
NYARA ZA SERIKALI
4
-
-4
+400
POMBE YA MOSHI.
48
24
+24
+100
WAHAMIAJI HARAMU
3
19
-16
-84
JUMLA
123
113
+10
+9

-          Kupatikana na silaha - Wilaya iliyoongoza ni Chunya  3 na Mbozi 2 .[Silaha aina ya  Gobole 6, Riffle 1 na Bastola ya  kienyeji 1]
-          Kupatikana na bhangi –Wilaya iliyoongoza ni Mbeya  21, Rungwe  7 na Chunya 7.  [Uzito wa Kilo 94 na Gram 734 pamoja na shamba moja la   bhangi yenye ukubwa warobo  hakari ¼ na miche 314 ]
-          Kupatikana na pombe ya  moshi[gongo] – Wilaya iliyoongoza ni Chunya 15, Mbeya 14  na Mbarali  4.[Ujazo wa lita 99 na mitambo 6]
-          Wahamiaji haramu –Wilaya iliyoongoza ni Mbozi 1/Momba 1na Mbarali 1.
[Wahamiajai haramu 28 - Somalia 4,Pakistan 7 na Ethiopia 17]

                    
MATUKIO YA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI CHA JAN-MACHI,  2014 NA JAN – MACHI, 2013.
MATUKIO
12,250
14,375
-2,125
-15
MATUKIO YA AJALI
98
156
-58
-37
AJALI ZA VIFO
58
65
-7
-11
WALIOKUFA
61
81
-20
-7
WALIOJERUHIWA.
104
91
+13
+14
AJALI ZA MAJERUHI
40
91
-51
-56
MAKOSA YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI
12,422
14,219
-1,797
-13
 TOZO [NOTIFICATION]
332,790,000/=
365,400,000/=
-32,610,000/=
-9


-          Matukio yote yaliyoripotiwa –Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 7,051, Mbarali 1,633  na Momba 1,142.
-          Matukio ya  ajali – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 51, Rungwe 14  na Mbarali 7.
-          Ajali za Vifo – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 20, Rungwe 14 na Mbarali 7.
-          Watu waliokufa –Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 22, Rungwe 17 na Mbarali 7.
-          Watu waliojeruhiwa - Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 65, Rungwe 13 na Kyela 9.

WITO WA KAMANDA:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati za wahalifu na uhalifu katika maeneo mbalimbali pale waonapo viashiria ambavyo si vya kawaida au pindi tukio linapojitokeza ikiwa ni kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno, mazungumzo ya simu au kwa kufika moja kwa moja kituo cha Polisi Kilipo Karibu na maeneo yao.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawahakikishia Wananchi/Wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Wageni wote hali ya Amani na Utulivu katika Kipindi hiki cha kusherehekea Sikukuu ya Pasaka. Kila Mwananchi aone anawajibu wa kufuata na kutii sheria zilizowekwa bila kushurutishwa. Pia rai kwa wananchi kuacha muangalizi/waangalizi nyumbani wanapotoka kwenda katika Ibada za Mkesha na Sherehe kwa jumla kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mali zao.

Kwa watumiaji wa Vyombo vya Moto wafuate na kuzingatia Sheria na Alama za Usalama Barabarani ili kuepuka ajali. Halikadhalika watembea kwa miguu kuwa makini na matumizi ya barabara ikiwa ni pamoja na kuvuka katika maeneo yenye vivuko [zebra crossing].

Aidha Kamanda wa Polisi anawataka wazazi/walezi kuwa makini na watoto wadogo kwa kutowaacha wakatembea bila uangalizi wa kutosha. Wamiliki wa kumbi za Starehe kuzingatia taratibu za uendeshaji wa Biashara zao ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya pia anatoa shukrani kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha kwa Jeshi la Polisi na kwa wananchi kwa njia ya kuhabarisha umma.

Nitumie nafasi hii kuwatakia Sikukuu njema ya Pasaka, kwa kuungana na Wakristu Dunia kote kusherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo.


 [AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Post a Comment