Ads (728x90)

MSHITAKIWA wa usafirishaji wa Mirungi(wa pili kutoka kulia) akiwa katika gari la Polisi akipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana

Washitakiwa wa makosa mbalimbali wakipelekwa mahabusu jana wakitokea kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mbozi

Mshtakiwa wa makosa ya usafirishaji wa Mirungi Joram Mwakalebela akielekezwa na askari kanzu kukaa chini baada ya kuahirishwa kwa kesi inayomkabili ya kukutwa na Mirungi kilo 80.

MSAFIRISHAJI maarufu wa mirungi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati Joram Mwakalalebela(48)(Sabas) ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya baadaye kufikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Mbozi kwa tuhuma za kukutwa na mirungi kilo 80.
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa njiani kuelekea nchi za Zambia hadi nchini DRC ambako amekuwa akifanya biashara ya usafirishaji mirungi kwa zaidi ya miaka 10.
Mwakalebela(48) ambaye ni mkazi wa Forest Jijini Mbeya amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilayani Mbozi mkoani Mbeya kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 80.
Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mbozi Rahimu Mushi, mwendesha Mashtaka wa Polisi Inspekta Samweli Sarro alisema kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo Januari 24 mwaka huu.
Alisema mshtakiwa alikutwa katika nyumba ya kulala wageni ya Jabari iliyopo Sogea mjini Tunduma majira ya saa 3:30 asubuhi akiwa na dawa za kulevya aina mirungi ikiwa katika mafungu 250 sawa na kgm 80.

Hata hivyo mshtakiwa alikana kosa hilo na kurejeshwa rumande hadi Februari 10 ambapo alipewa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye nyumba zisizohamishika na fedha taslimu kiasi cha sh. milioni 5.
‘’Alikutwa katika nyumba ya kulala wageni ya Jabari ipo kitongoji cha Sogea mjini Tunduma, mirungi ilikua katika vifurushi vya mafungu 250 ni sawa na kilo 80,’’alisema Inspekta Sarro.
Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa mjini Tunduma wanadai kuwa kilo moja ya Mirungi ni sawa n ash.40,000 hivyo kiasi hicho cha mirungi kilichokamatwa ni zaidi y ash. Milioni 3.



Post a Comment