Ads (728x90)

Ni siku ya pili kwa  wapanda baiskeli wanaomuunga mkono JK kutimiza miaka 10 ya uongozi wake maarufu kwa jina la Ahsante JK au Appriciate Tanzania mmoja wa waendesha baiskeli hao Wiseman Luvanda akiwa amesimama na kupumzika kidogo akiwa njiani kuelekea mkoani Njombe mjini Makambako.

Safari inaendelea


Kuna wakati mwingine wapanda baiskeli hao walilazimika kukaa barabarani kutokana na uchovu wa safari na mara nyingine kuchimba dawa.
Na kwa kuthibitisha uzalendo wao kwa nchi yao vijana hao watatu ambao wamedhamiria kuelekea Ikulu kukutana na JK na kumpongeza kutimiza miaka 10 ya uongozi wake,wametimiza haki yao ya kujiandikisha kupigia kura ambazo
   

Wapanda baiskeli hao waliendelea na safari yao huku wakikatisha milima na mabonde kuelekea Jijini Dar es salaam.
   

Kuna wakati mwingine walilazimika kupumzika na kupiga mbonji walau kwa dakika 10, safari inaendelea
 

Ili kujidhihirisha kuwa wako katika mazingira halali na kuhitaji sapoti kutoka kwenye vyombo vya usalama wapanda baiskeli hao walifika hadi kwenye ofisi ya Mkuu wa Polisi katika kituo cha Makambako.
Kazi na dawa wapanda baiskeli hao walikamilisha safari yao kwa kupumzika na kupata chakula mjini makambako.
Kazi na Dawa
Makambako
 

Post a Comment