Ads (728x90)

Kitabu maalum cha wapanda Baiskeli kutoka Mbeya ambacho atakabidhiwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kukamilisha safari yao km 830 kutoka Mbeya hadi Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwapa nasaha wapanda baiskeli watatu kabla ya kuelekea Jijini Dar es salaam kwa kutumia Baiskeli kwa ajili ya kumuunga mkono na kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kutimiza miaka 10 ya uongozi wake.


Mmoja wa wapanda Baiskeli akionesha mbwembwe za uendeshaji wa baiskeli kabla ya kuanza safari mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro


Wapanda Baiskeli wakianza safari ya kuelekea Dar es salaam kutokea Mbeya wakiadhimisha kauli mbiu yao waliyoiita Asante JK kumaliza miaka 10Mmoja wa wadhamini wa wapanda Baiskeli hao Sambwee Shitambala kupitia kampuni yake ya Shitambala Advocate and Company akiwaaga wapanda baiskeli hao ambao wanatarajia kutumia siku nane kuelekea Jijini Dar es salaam kukutana na Rais Jakaya Kikwete kumpongeza kwa kutimiza miaka 10 ya uongozi wake.

 

Post a Comment