Ads (728x90)

Diwani wa kata ya Songwe Ayasi Njalambaha akimkabidhi cheti mmoja wa maskauti waliohitimu mafunzo ya miaka miwili kambo ya Songwe Magereza
Diwani wa kata ya Songwe Ayasi Njalambaha  akitoa nasaha baada ya kukabidhi vyeti vya mafunzo kwa wahitimu wa Skauti Songwe


Baadhi ya Skauti waliohitimu mafunzo ya skauti jana
Kaimu Mkuu wa magereza wa Songwe Saleh Hassan akitoa nasaaha wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti maskauti waliohitimu mafunzo ya miaka miwili  jana



Mkufunzi wa mafunzo ya Skauti Deogratius Mazengo akimkaribisha mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Songwe Ayasi Njalambaha kwa ajili ya kitendo cha kuapisha wahitumu wa mafunzo ya Skauti.

WAHITIMU wa mafunzo ya miaka miwili ya Skauti wilayani Mbeya wametakiwa kutumia mafunzo ya miaka miwili waliyopata kwa kulinda amani na utulivu wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na kutojiingiza katika vikundi vya uhalifu.
‘’Mafunzo yenu yalenge kuisadia jamii na kutumia mbinu mlizopata kwa ajili ya kujiletea maendeleo yenu wenyewe’’alisema Diwani wa Kata ya Songwe Ayasi Njalambaha.
Njalambaha pia aliwataka wahitimu hao kumtanguliza Mungu katika utendaji wao katika jamii ili kujijengea imani ya Mwenyezi Mungu na kuwa daima kila mwenye imani hutenda haki.
‘’Mtangulizeni Mungu kwenye kazi zenu huko mbele ya jamii, ukimtanguliza Mungu utakuwa na imani, ukiwa na imani utatenda haki, tunaporudi katika maeneo yetu tusaidie kudumisha amani na utulivu,’’alisema Njalambaha.
Aidha Njalambaha aliwaasa wahitimu hao kutojihusisha na ubaguzi unaohusisha  makundi ya itikadi za kisiasa ama ya kidini na kwamba wanatakiwa kutanguliza uzalendo na kusaidia maendeleo ya nchi yetu bila ubaguzi.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Magereza wa Gereza la Songwe Salehe Hassan Saleh aliwataka wazazi kutoa ushirikiano kwa vijana wanaojiunga kwenye mafunzo ya Skauti kwa kuwa mafunzo hayo mbali na kuwajengea uwezo na uelewa huwapa ujasiri na ukakamavu.
Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo Deodatus Mazengo alisema kuwa mafunzo hayo yaliwahusisha skauti 47 waliopata mafunzo ya miaka miwili ambao  wametokea katika vijiji vilivyopo kata ya songwe wilaya ya Mbeya.


Post a Comment