Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)Nicholas Musonye akikagua uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine leo asubuhi |
Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye akiweka kumbukumbu katika kalabrasha lake baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa MREFA Elias Mwanjala kwenye uwanja wa Sokoine leo asubuhi |
Baadhi ya waandishi wa Habari wakizungumza na Katibu Mkuu wa CECAFA katika uwanja wa Sokoine leo asubuhi |
Katibu wa CECAFA Musonye akiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi alipotembelea uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine leo |
Mkurugenzi wa Ufundi TFF akitoa maelekezo mbele ya Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye na waandishi wa habari leo asubuhi kwenye ofisi za chama cha Mpira wa Miguu MREFA ndani ya uwanja wa Sokoine |
SHIRIKISHO la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limesifu jitihada za timu ya soka ya Mbeya City kwa kubadilisha muelekeo wa ushabiki na kuiweka ramani ya soka nchini kwa kuuondoa ushabiki wa soka uliozoeleka wa kushangilia timu za Simba na Yanga.
Akizungumza
Jijini Mbeya Katibu Mkuu wa (CECAFA) Nicholas Musonye alisema kuwa Tanzania
ilizoeleka kwa ushabiki wa timu za Yanga na Simba, na kwamba kuibuka kwa timu
za mikoani kumeleta changamoto mpya ya taswira ya kukua kwa soka nchini.
‘’Ushabiki
wa Simba na Yanga naona umeanza kupungua baada ya kuibuka kwa Mbeya City,
jitihada hizi tutazienzi ili kukuza kiwango cha soka katika nchi zetu za Afrika
Mashariki na Kati,’’alisema Musonye ambaye pia ni mratibu wa Shirikisho la
vyama vya Mpira wa Miguu Afrika CAF.
Musonye ambaye
alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi alisema kuwa
CECAFA imeichangua timu ya Mbeya City kushiriki katika michuano ya Kombe la
CECAFA la nchi zinazozunguka mto Nile(CECAFA NILE CUP) ambazo zinazotarajiwa
kuanza Mei 22 na kumalizika Juni 4 katika makundi manne nchini Sudan.
Musonye
alitaja makundi hayo kuwa ni Khartoum ambako kutakuwa na vituo viwili vya
mashindano,Port Sudan kituo kimoja na Al Shanti ambapo jumla ya timu 16
zitashiriki mashindano hayo.
Alizitaja
timu hizo na nchi zake katika mabano kuwa ni El mereikh, Al Shant na El
Arab(Sudan),Victoria University(Uganda)Defence(Ulinzi)(Ethiopia),Mbeya
City(Tanzania Bara)Polisi(Zanzibar)
Polisi(Ruanda) Ports(Djibout) Elmas(Somalia) AFC Leopard(Kenya),Flambeau(Burundi)
na Ismailia na Arab Contractors(Misri).
Katika hatua
nyingine Musonye ambaye aliukagua uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine aliwataka
viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya kuendelea kuukarabati uwanja
huo ili uweze kukidhi viwango vya michezo ya Kimataifa.
‘’Endeleeni
kuumarisha uwanja wenu, nimeuona, mambo mengine yapo kiutawala nitapeleka
ripoti yangu CECAFA,’’alisema bila kufafanua Musonye.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mbeya Elias Mwanjala
alisema kuwa ujio wa CECAFA mkoani Mbeya unatia moyo wa kuendelea kuukarabati
uwanja huo ili ikiwezekana ukubalike katika michezo ya Kimataifa.
‘’Tunashukuru
kupata fursa hii naona tumeanza kuungwa mkono Kimataifa, tunaendelea kuthamini
mchango wa TFF kwetu, tupo katika mikakati wa kuufanya uwanja wa Sokoine uwe ni
wa Kimataifa,’’alisema Mwanjali.
Post a Comment