Ads (728x90)


Wananchi walijitokeza kwa wingi katika maandamano ya kilele cha siku ya Red Cross yaliyofanyika Kitaifa Jijini Mbeya, waendesha Boda boda walishiriki mandamano.
 





Maandamano hayo yaliyoanzisha Mafiat na kupita barabara kuu ya Dar-Zambia kiasi cha mwendo wa km 2 yaliongozwa na Brass Band ya Magereza ya Mkoani Mbeya.



Vijana wa Skauti walishiriki maandamano hayo.


Mamia ya wakazi wa Jiji la Mbeya walishiriki maandamano hayo ya kilele  cha maadhimisho ya siku ya Msalama Mwekundu Duniani ambayo Kitaifa yalifanyika Mkoani Mbeya.

Baadhi ya waandishi wa habari  walishiriki katika kupata taarifa za maadhimisho hayo

Makamu wa Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Dkt. Zainab Gama akisoma risala maalum ya chama cha Msalaba mwekundu nchini

Mwandishi wa Habari mwakilishi wa Kampuni ya Business Times Charles Mwakipesile akipokea kadi ya Uanachama kutoka kwa Mgeni Rasmi aliyemwakilishi Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid, Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro.

Mwandishi wa Habari Mwakilishi wa TBC mkoani Mbeya Hosea Cheyo akiwa na cheti cha Heshima cha kuthaminini ushiriki wa chombo hicho kwenye maadhimisho hayo.

Emmanuel Lengwa mwakilishi wa ITV/Redio One na Hosea  Cheyo Mwakilishi wa TBC wakiwa na vyeti vya heshima siku ya Red Cross mkoani Mbeya.


Wanahabari wakibadilishana mawazo wakati wa kilele cha maadhimisho hayo.


Nderemo na Vifijo viliendelea hadi saa mbili usiku wakati wa ugawaji wa zawadi kwa timu za mpira wa miguu zilizoshiriki katika michezo kwenye wiki ya Msalaba Mwekundu.


Wananchi wakijimwaga mwaga kwenye maadhimisho ya kilele cha sherehe za Msalaba mwekundu mkoani Mbeya



Post a Comment