Kikosi cha timu ya Taifa Malawi kitakachokutana na Stars dimmba la Sokoine kesho |
Kocha mkuu wa timu ya Taifa Malawi Young Chimodzi akitaja orodha ya waachezaji wa timu ya Taifa Malawi watakaoingia dimbani na timu ya Taifa uwanja wa Sokoine kesho |
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali Jijini Mbeya wakifuiatilia kwa makini taarifa za kocha mkuu wa timu ya Malawi |
Kapteni wa timu ya Malawi James Sangala akizungumza namna walivyojipanga kushinda katika mechi ya kesho na Taifa Stars. |
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Malawi inayotarajia kuchuana na timu ya Taifa Stars Young Chimodzi amesema wanayo matarajio makubwa ya kushinda mechi ya Kirafiki ya Kimataifa inayotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Hotel ya Mkulu Jijini Mbeya leo asubuhi Chimdodzi alisema kuwa wamejipanga vyema katika mchezo huo ili kuweka matumaini ya kucheza vyema katika michuano ijayo.
''Hii kwetu ni mechi kubwa, itajenga uwezo kwa timu yetu, tumejipanga kufanya vyema ili kuijengea heshima nchini yetu,''alisema Chimodzi.
Alikitaja kikosi kitakachochuana na Stars kuwa ni Magolikipa wawili ambao ni Charles Swini anayechezea timu ya Silver Strikers ya nchini Malawi na Richard Chipuwa anayechezea Wanderers FC, wengine ni walinzi majina ya timu zao kwenye mabano ni Pilirani Zonda(EPAC FC),Francis Mulimbika(Wanderers FC) na John Lanjesi(Civo FC).
Aliwataja walinzi wengine kuwa ni Emmanuel Zoya(Civo FC) Bashiri Maunde (Tiger FC) na George Nyirenda(Big Bullet FC).
Walinzi wa kati ni John Banda na Mecium Mhone wanaochezea klabu ya (Blue Eagles) Douglas Chirambo-Big Bullets FC,World Nkuliwa(Kamuzu Barracks FC), Frank Banda na Junior Chimodzi(Silver Strikers FC) Philip Masiye Blue Eagles (FC) na Ndaziona Chatsalira(Silver Strikers FC).
Kocha Chimodzi aliwataja washambuliaji kuwa ni Gaston Simukonda(Moyale FC), Green Harawa(Silver Strikers FC,Diverson Mlozi(Big Bullets FC) na Rodrick Gonani(Silver Strikers FC).
Timu hiyo iko katika msafara wa jumla ya wachezaji na viongozi 32 wakiwemo kocha msaidizi Jack Chamangwana, Meneja wa timu Franco Ndawa, Ofisa wa timu James Sangala, Daktari Gift Banda, kocha wa magolikipa Philip Nyasulu, Mkuu wa msafara Flora Mwandira na viongozi wa kamati ya Ufundi John Anisa na Jossan Namwera na madereva wawili.
Timu hiyo Taifa ya Malawi inatarajia kucheza na Timu ya Taifa Stars ambayo iko kambini kwa takribani wiki mbili mkoani Mbeya ikijiandaa kwa michuano mbalimbali ya Kimataifa.
Post a Comment