Ads (728x90)

Kama mjali, wa taa, maisha yalivyo,
Ni muhali, kukaa, vivyo ulivyo,
Kwa kila uwakavyo, huisha vivyo.

Maisha kama tambara, bovu, liishavyo,
Hayahitaji papara,na nguvu isivyo,
Kadri uishivyo, ndivyo yaishavyo.

Uishi vyema, na watu,kadri ilivyo,
Uwe mwema,kwa utu, daima ndivyo,
Ya dunia ndivyo, maisha yalivyo.

Uwe na njema, tabia, uendavyo,
Ichunge huruma,zingatia, uwezavyo,
Ya akhera ma'ndazi, wako ujuvyo.

Ibada kwako, ni hima, si ya upuuzo,
Kuikosa mwiko, lazima, marejelezo,
Zingatia makatazo, ya Karima.

Kwa magego, ukamate, iwe zingatio,
Siupe mgongo, ujute na muishio,
Hapa malizio, kwa waadhi huno.

WAKATABAHU.

Post a Comment

  1. Nimepita kibarazani kwako, nimevutiwa na vilivyomo. Kazi nzuri kaka, tutembeleane!

    ReplyDelete
  2. Fasihi za ufasaha zenye fasaha zake. Ukurasa mwingine wa blogu umeingia, kazi mpya yenye uhalisi. Inavutia kuendelea kuwa kwenye ulimwengu huu wa blog.

    ReplyDelete