Ads (728x90)

TA, TE, TI, TO, TU.

TA:Nataataa na tata,watatue watatuzi,
Sitati kimtang'ata, kwa tata za utatizi,
Nitatapo Kimvita,watatwao watatezi,
Mahiri wa utatizi, tutete na tungo TATA.

TE: Niteetapo na tete, siteti penye terezi,
Hateta hadi utete, nitete na watetezi,
Nije teta kiutete, nimetemete ja mwezi,
Mahiri wa utatizi, tutete na tungo TATA.

TI:Ja burudi ya tikiti, tungo njema ndizo hizi,
Lahamu yake ya kati,ni tamu kushinda ndizi,
Ulilapo katikati, watarazia uchizi,
Mahiri wa utatizi,tutete na tungo TATA.

TO:Natongoa mitopoto, ilotopea kwa kwa wazi,
Kauli za kilipyoto,zatotesha fasihi enzi,
Beti tele za upoto, kurasa zinabarizi,
Mahiri wa utatizi, tutete na tungo TATA.

TU:Tamati Ta, Te, Ti,To, Tu,tungo TATA sendelezi,
Sijateta kwa mtutu, bali tati za ujuzi,
Kuwafunda watukutu, fasihi wasomaizi,
Mahiri wa utatizi, tutete na tungo TATA.

Wakatabahu

Post a Comment

  1. Mkwinda: umekuja na mpya kabisa. Ta, te, ti, to, tu. Sawa malenga wetu. Usiwe unapotea namna hii.

    ReplyDelete
  2. NDA: Nda kauliyo Mkwinda hinitiya mato giza
    NDE: Mamvitani chonde chonde, nti huno hutereza,
    NDI:Fasihi haina mshindi, na wamrima waiweza,
    NDO: Hisikiyapo ndo ndo ndo, nsondo huno sitateza
    NDU: Watukutu si watundu, ntundu hucha kujikweza
    Nda! nde! ndi! ndo! ndu! mdundo, Ubeti watosheleza,
    Ndiye nzuri wa nyendo, kurasa nacha kujaza

    ReplyDelete
  3. asante Mwandani,kwa fikrezo makini,
    mpashe mkwindani,amekuwa mwanajini,
    mara ta mara ten,kama yuko mautini,
    anatatarika nini,ka sio malengani!

    kwa nini anajihini,kutunganiblogun
    ndesanjo yu mashakan,kuingia hatiani,
    ni sawa na kumkundi,nje mwa kasrini
    anatatarika nini, ka sio malengani!

    wa zenjin mrimani,hata kule mombasani,
    kote tumo utatani,kwa hii tata tatani,
    nashindwa pata baini,nini hasa atungani,
    anatatarika nini,ka sio malengani!

    sasa makene baini,umtoe tatarani,
    kijana wako shetani,aso haya wala soni,
    si mwingine rashidani,aondoka ulengani
    anatatarika nini,ka sio malengani

    naondoka postini,ni mgeni fasihini,
    sije anza chokoani,bata akanishindani
    Mkwinda sasa adhini,nami tayari swalani,
    anatatarika nini,ka si malengani

    ReplyDelete
  4. mh!
    kazi kwelikweli,hii fani itabidi niulize chuo chake maana yataka moyo,ta te ti to tu,nda nde ndi ndo ndu,
    inawezekana wameanza kutafuta maana ya blog kwa njia ushairi hawa tuendelee tuone!

    ReplyDelete
  5. mzee pink noma. chagua color ya kiume.

    ReplyDelete
  6. Nimekuona Nyembo, kwa zako nyimbo,
    Lakini ndio mwendo,bali acha majigambo,Ukiingia katika fani, utanata kama urimbo,usijifutue ja Tembo, ukaharibu huu mtambo.

    Huu ni ghali mtambo,
    Asiliye ni ng'ambo,
    Hivyo chukua tahadhari Nyembo.

    Tulia nakujia na kitu kingine nadhani ni kweli tuko katika safari ya kulisaka neno mbadala kwa hili la Blogu tulia sikia vyombo tazama katika blogu kuna CHACHANDU ZA UCHACHIZI.

    ReplyDelete