Ads (728x90)

Mbunge wa jimbo la Nzega Dkt.Hamisi Kigwangala ameonyesha ukomavu wa kisiasa, moyo wa kujiamini na kujitambua kama Mwakilishi wa wananchi na siyo mwakilishi wa chama chake kwa maana ya CCM!

Mh Kigwangala ameandaa maandamano makubwa ya amani kwa kuwashirikisha wananchi wote wapenda maendeleo aidha maandamano haya yameahidiwa kufanyika siku japo amekuwa akipata upinzani mkali toka kwa ccm kwa sababu ccm isingependa kumuona Mbunge wake akiandaa maandamano ya kupinga jambo ambalo linasimamiwa na serikali iliyopo madarakani kwa maana ya ccm yenyewe.

Mh kigwangala baada ya kutangaza kuandaa maandamano hayo amepata upinzani mkali kutoka kwa uongozi wa ccm wa wilaya yake juu ya kuyazuia maandamano hayo hali iliyofikia kumita Mh Kigwangala kwenye kikao cha kamati ya Maadili ya ccm kitu ambacho Mh Mbunge aliona kuwa hatendewi haki na kugoma kutokea mbele ya kamati hiyo.

Katibu wa ccm wilaya ya nzega baada ya kuona kuwa amedharauliwa akaamua kumuandikia Mh Mbunge barua ya kumzuia kufanya maandamano hayo barua ambayo baadae imeonekana kwenye mtandao wa kijamii wa facebook unaotumiwa na Mh Kigwangala japo hadi dakika ya mwisho Mh Mbunge amesisitiza kufanya maandamano hayo.

Nimeamua kumpongeza Mh kigwangala kwa maamuzi yake hayo ili kuwafundisha wabunge wengine wote wanapaswa kuwajibika kwa wapiga kura wao na si kwa chama kilichowapeleka Bungeni na hapa naanza kupata ladha ya kuwa na wagombea binafsi kwani inamfanya mchaguliwa kuwajibika zaidi kwa wananchi na si kwa chama cha siasa, kigwangala kaonyesha njia nadhani na wabunge wengine watafuata wachache walionyesha njia safi ya uwajibikaji kwa wananchi ni pamoja na Mh Fulikunjombe, kangi Lugola na wengineo.

Kwa mara nyingine tena hongera sana Mh Kigwangala kwa kuipinga CCM kwa maslahi wana Nzeoga wakiwemo wana CCM wanaokuzuia kufanya maandamano hayo.

Ifuatayo na nakala ya barua aliyoandikiwa Mh kigwangala inayopatikana kwenye mtandao wa Mh Kigwangala.


Post a Comment