Ads (728x90)

Waziri wa Usalama wa Kenya, Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode, wamefariki katika ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Ngong, nje ya Nairobi.
Profesa George Saitoti
Abiria wote saba waliokuwa kwenye ndege hiyo waliteketea kwa kiasi wasichoweza kutambulika.
Makamo wa rais wa Kenya, kalonzo Musyoka, alipofika kwenye tukio la ajali alitoa rambi-rambi zake na alieleza wale waliokuwamo ndani ya ndege ambao wote wameteketea:
"Ndege hiyo ya aina ya Eurocopter ya police airwing, ambayo ilikuwa inaelekea Yugis, ilikuwa imembeba Waziri George Saitoti, naibu waziri Orwa Ojode na maafisa rubani wa ndege, Nancy Gitwanja na Luke Oyugi, na vilevile askari wawili ambao wanakuwa wanaandamana na Waziri Saitoti, Inspector Tonkei na Thomas Murimi"
Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Waziri Saitoti ni msiba mkubwa kwa nchi.
Na Waziri Mkuu Raila Odinga, ambaye piya amefika kwenye ajali amesema, kifo cha Bwana Saitoti kinasikitisha na ni pigo kwa taifa.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema waliona helokpta hiyo ikiyumba-yumba na iliripuka na kuwaka moto alipogonga ardhi.
Bwana Saitoti aliwahi kuwa makamo wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Alikuwa na umri wa mika 67....CHANZO BBC SWAHILI


Post a Comment