OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/B/130 25 Mei, 2012
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo
ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002
kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu
wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la
kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 2285 za
kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sanyansi na
Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Msajili Mahakama ya Rufaa, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Lindi,
Manyara, Kigoma, Arusha, Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Tabora, Morogoro na
Rukwa.
Katibu Tume ya Utumishi wa Umma, Katibu, Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, Katibu Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Katibu
Tume ya Pamoja ya Fedha, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji,
Msajili wa Vyama vya Siasa, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA),
Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania, Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za
Ajira Tanzania, Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
2
Halmashauri ya Jiji la Dar
es Salaam na Mwanza. Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Mtwara, Singida,
Sumbawanga, Morogoro, Songea, Kigoma/Ujiji na Temeke. Halmashauri ya Wilaya ya
Babati, Bunda, Chato, Chamwino, Handeni, Songea, Bahi, Kibaha, Pangani,
Tunduru, Mkuranga, Mafia, Mufindi, Njombe, Mwanga, Nachingwea, Nkasi, Masasi,
Monduli, Mtwara, Ruangwa, Rufiji, Bukoba, Tandahimba, Same, Tarime, Kibondo,
Biharamulo, Newala, Simanjiro, Kondoa, Ngara, Mpanda na Halmashauri ya Mji wa
Njombe.
NB: Aidha, tangazo hili linapatikana kwenye
tovuti zifuatazo: www.ajira.go.tz, www.utumishi.go.tz na www.pmoralg.go.tz
1.0 AFISA UTUMISHI DARAJA LA II (HUMAN RESOURCES OFFICER
GRADE II) – NAFASI 30
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na
Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Tume ya
Utumishi wa Umma, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Rukwa. Halmashauri ya Manispaa
ya Mtwara na Singida, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Rufiji, Handeni, Mkinga,
Ngara, Songea, Bahi, Newala na Halmashauri ya Jiji la Mwanza
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutunza Kumbukumbu sahihi za watumishi wote katika Wizara,
Mikoa, Wilaya na Idara zinazojitegemea kulingana na mahali alipo.
Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya
utumishi.
Kutafiti, kuchanganua na kukadiria idadi ya watumishi
wanaohitaji mafunzo.
Kuandaa na kupanga mipango ya mafunzo ya muda mfupi na
mrefu.
Kukadiria na kupanga mahitaji ya vifaa vya mafunzo kwa
kushirikiana na vyuo vilivyopo chini ya sekta zinazohusika.
Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na kumbukumbu zote
zinazohusu mipango ya watumishi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi Jamii au Sanaa
kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao wamejiimarisha
(major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
§ Menejimenti
ya Raslimali Watu (Human Resources Management).
§ Elimu
ya Jamii (Sociologly).
§ Utawala
na Uongozi (Public Administration).
§ Mipango
ya Watumishi (Manpower Planning).
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
3
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa
mwezi.
2.0 AFISA TAWALA DARAJA LA II (ADMINISTRATIVE OFFICER GRADE
II) – NAFASI 14
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Katibu Tawala
Mkoa wa Tanga, Pwani, Lindi, Mtwara, Manyara, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya
Njombe.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusajili vizazi, vifo na ndoa na kutoa hati za viapo.
Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu,
Kuwapokea na kuwahoji wakimbizi wanaowasili,
Kuweka kumbukumbu za Wakimbizi
Kutunza na kugawa vifaa vya wakimbizi katika makazi.
Kuainisha, kuchambua na kushauri kuhusu matatizo ya
wakimbizi.
Kusimamia nidhamu ya wakimbizi.
Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu
mbalimbali Serikalini kutegemeana mahali alipo.
Kusimamia kazi za utawala na uendeshaji katika ofisi za
Serikali.
Kutoa vitambulisho kwa wakimbizi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:- Utawala, Elimu ya jamii,
Sheria (baada ya internship), Menejimenti ya Umma
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa
mwezi.
3.0 AFISA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (RECORDS OFFICER GRADE II)
– NAFASI 2
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi hivyo atafanya kazi kwa
maelekezo ya Maafisa Kumbukumbu walio juu yake kwa cheo. Kazi atakazojifunza na
kufanya ni zile zifanywazo na Afisa Kumbukumbu Daraja la I:-
Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, kutunza, na kusimamia
matumizi ya kumbukumbu.
Kutambua na kutafuta kumbukumbu katika masjala.
4
Kudhibiti
mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa na kompyuta, kutunza na kusimamia matumizi
yake.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji
na Uhifadhi wa Kumbukumbu (Records management & Archieves), Upimaji na
Ramani na nyingine zinazolingana nayo kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa
na Serikali. Aidha wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa
mwezi.
4.0 MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II) – NAFASI 14
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Katibu Tawala Mkoa wa Lindi,
Rukwa, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,
Tunduru, Rufiji, Mkuranga na Newala.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya na
kuratibu takwimu
Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa
kuchukua takwimu za mfano/vielelezo (Sampling)
Kukusanya, Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu au
Hisabati au sifa zinazolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na
Serikali na wenye ujuzi wa kutumia “Information Communication Technology (ICT)
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa
mwezi.
5.0 MTAKWIMU MSAIDIZI (ASSISTANT STATISTICIAN ) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya Takwimu ( Data)
Kuchambua na kukagua fomu za maswali zilizokwishajazwa na
kujibiwa.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti (Certificate) cha Takwimu kutoka Chuo
cha Takwimu cha Afrika Mashariki (The Eastern Afrika Statistical Training
Center) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali wenye ujuzi wa kutumia
kompyuta (ICT)
5
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa
mwezi.
6.0 KATIBU WA KAMATI DARAJA LA II (COMMITTEE CLERK GRADE II)
– NAFASI 13
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani,
Mkinga, Tunduru, Mwanga, Newala, Mkuranga na Nkasi.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa ratiba ya vikao vyote vya Halmashauri na kamati
zote kwa kushauriana na Mkurugenzi Mtendaji
Kuandika Mihutasari ya vikao vya Halmashauri
Kuweka Kumbukumbu za vikao vya Halmashauri nma kamati zake.
Kutunza Vifaa vyote vinavyohusiana na mikutano.
Kuhifadhi orordha ya mahudhurio ya Madiwani na Wataalamu.
Kutoa ratiba ya ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio
Kutunza Kanuni za Mikutano.
Kusimamia “cutting” za mihutasari.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada /Stashahada ya Juu ya Sheria/Sanaa/
Utawala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGS D kwa mwezi.
7.0 AFISA MIPANGO MIJI DARAJA LA II (TOWN PLANNER) – NAFASI
17
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Tabora, Rukwa,
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mtwara, Singida, Sumbawanga, Halmashauri
ya Wilaya ya Babati, Handeni, Nachingwea, Rufiji, Mafia, Morogoro, Pangani na
Tunduru.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa mipango ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela.
Kuandaa michoro ya Mipangomiji.
Kupokea michoro ya Mipangomiji na taarifa za maeneo ya
ardhi yanayopendekezwa kuiva kwa ajili ya uendelezaji kimji.
Kuchambua takwimu na taarifa kwa ajili ya maandalizi ya
mipango mipya ya makazi.
Kupokea na kuweka kumbukumbu za maombi ya mabadiliko ya
matumizi ya ardhi na umegaji wa viwanja.
Kuhakikisha kuwa mabadiliko ya matumizi ya ardhi
yanaingizwa katika michoro.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
6
Kuajiriwa mwenye Stashahada
ya juu/Shahada katika fani ya Mipangomiji kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi au Vyuo
Vikuu au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa
mwezi.
8.0 MSAIDIZI WA MTENDAJI MKUU DARAJA LA II (EXECUTIVE
ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri
Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa.
Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni,
tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa
kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati
unaohitajika.
Kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu
chochote kinachoitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
Kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake
na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
Kuyapokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika
sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusikika.
Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
mahali alipo.
Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi na kuifikisha
sehemu zinazohusika na upatikanaji wa vifaa hivyo.
Kuwapangia na kuwaelekeza kazi Makatibu Mahsusi walio chini
yake.
Kuwasaidia Makatibu Mahsusi walio chini yake kuhusu
matumizi ya mashine za kazi na utunzaji wake.
Kutoa na kufuatilia panapohusika kuhusu matengenezo ya
mashine za kazi.
Kuandika muhutasari wa vikao vinavyohusika sehemu alipo na
kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya vikao hivyo.
Kuandika barua zinazotoa taarifa ya ratiba ya shughuli au
safari za Mkuu wake na kuitisha vikao.
Kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wake sehemu
mbalimbali
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Stashahada ya kawaida ya Uhazili itolewayo
na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) au chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali ambaye amehudhuria mafunzo ya kompyuta na kupata cheti katika
programme za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
Pia, Awe na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka kumi na mbili. Aidha, Awe
Amehudhuria na kufaulu mafunzo
7
ya Menejimenti kwa ajili ya Wasaidizi wa Watendaji Wakuu
kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS F kwa
mwezi.
9.0 AFISA USIMAMIZI WA FEDHA DARAJA LA II (FINANCE MANAGEMENT
OFFICER II) - NAFASI 2
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga na
Mtwara
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandikisha na kudhibiti Amana (Securities) za Serikali.
Kufuatilia hati za hisa.
Kuwasiliana na watoaji mikopo/misaada kuhusu maendeleo ya
utekelezaji wa miradi.
Kuweka kumbukumbu za madeni ya nje.
Kuweka kumbukumbu za mikopo ya ndani.
Kufuatilia na kusimamia matayarisho ya makadirio ya mapato
na matumizi ya Serikali.
Kufuatilia utayarishaji na uchambuzi wa “Flash Reports” za
kila mwezi.
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo mkubwa
katika fani ya Uchumi na Mipango (Major in Economics) au Biashara au Sheria
(LL.B) au Stashahada ya Juu ya Uhasibu au Uchumi & Mipango au Biashara au
Stashahada ya juu ya Usimamizi wa kodi kutoka Chuo/Taasisi inayotambuliwa na
Serikali.
Waombaji wenye Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa
nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na NBAA watafikiriwa kwanza.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGS.D kwa mwezi
10.0 MHAKIKIMALI DARAJA LA II (STOCK VERIFIER GRADE II) -
NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukagua bohari za kati za Serikali na kutoa taarifa za
ukaguzi.
Kutathmini na Kuchambua hoja muhimu zilizomo katika taarifa
za uhakikimali.
Kufanya uchambuzi wa taarifa za ‘Boards of Survey’ na kutoa
mapendekezo juu ya utekelezaji wake.
Kutunza daftari la taarifa za upotevu, ajali, fidia,
vitunzia fedha (cash receptables), usajili wa magari ya Serikali na uahalisho
(respective approval).
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
หนังแอคชั่น หนังใหม่ ดูหนังฟรีต้อง Alita: Battle Angel อลิตา แบทเทิล แองเจิ้ล (2019) สนุกกว่าใครที่เว็บดูหนังเว็บนี้
ReplyDeletehttps://www.doonung1234.com/