WAANDISHI
wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wamekutana jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kuunda Mtandao utakaoweza kusimamia, kupigania pamoja na kutetea haki
zao.
Akizungumza
katika kikao hicho juzi Katibu wa muda aliyeteuliwa na waandishi hao, Eneza
Mende alisema kuwa mtandao huo utajulikana kwa jilna la‘Waandishi wa Habari
Tanzania ‘ (TAJONET).
Alichanganua
kuwa mtandao huo hutatumika kama chachu ya kusaidiana katika matatizo
mbalimbali, ukiwa na sauti moja katika kutetea maslahi yao, huku ukihusika moja
kwa moja katika kusimamia maadili ya tasnia ya habari ambayo yanadaiwa
kuporomoka.
Mende
alisema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wandishi wa habari kujikuta
wakikabiliwa na matatizo mbalimbali huku wakikosa msaada.
Aidha,
alibainisha kuwa TAJONET utakuwa bega kwa bega katika kuangalia suala zima la
afya ya wananchama kwa kuangazia ngazi ya chini kama matibabu awapo
hospitalini, pamoja na msiba.
“Watu
wengi wamekuwa wakichukulia matatizo ni kifo, bila kuangalia mambo mengine kama
ugonjwa, sisi hatutaki kujielekeza hivyo bali tunataka ltatizo la ugonjwa
lipewe kipaumbele ili kuepusha vifo visivyo na ulazima”alisema Mende.
Aidha,
Mkutano huo umeteua viongozi wa muda 14, ambao kati yao wataunda kamati ya
rasimu ya upatikanaji wa katiba ya mtandao huo ambapo watakutana tena Julai 5
mwaka huu.
Imewekwa
na Dotto Mwaibale
Post a Comment