Ads (728x90)

Ujumbe mzito wa Bill & Melinda Gates Foundation kutoka Marekani ukiongozwa na Senior Programme Officer (Market Access) Richard Rodgers ulitua leo kwa ndege ya kukodi kwenye ofisi za Kapunga Rice, Chimala na kufanya mazungumzo na George Mtenda wa Mtenda Kyela Rice Supply Company ya Mbeya.
 
Rodgers alifuatana na Karen Harkono na Niraj Varia na kwa upande wa Mtenda Kyela Rice wawakilishi walikuwa Emile Malinza, Josiah Nyato na Jesko Linga.
 
Gates Foundation waliridhika na maelezo yakinifu kutoka Mtenda Kyela Rice na wameahidi kusaidia katika nyanja za mafunzo kwa wakulima na upatikanaji wa pembejeo za kilimo.
 
Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea na mwelekeo utapatikana baada ya miezi minne kuanzia sasa kwani Rodgers ameahidi kuwasiliana na ofisi zao za Marekani na kuwapa mrejesho wa ziara yake.
 

Post a Comment