Ads (728x90)





















Na, Rashid Mkwinda, Mbeya

MTU mmoja amekufa papo hapo na wengine 11 kujeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Nzovwe jijini Mbeya baadaa ya Lori aina ya Leyland DAF kufeli breki na kuzigonga kwa nyuma Hiace mbili zilizokuwa zikifanya safari zake kati ya Mwanjelwa na TAZARA.

Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa lori hilo lenye namba za usajili T 721 BVD na Trela lenye namba T 668 BGZ lililokuwa likielekea barabara Zambia liliigonga Hiace yenye namba  T 945 AFG ambayo nayo iliigonga Hiace nyingine yenye namba za usajili T 150 AJL ambazo zote zilikuwa zimesimama kwa muda eneo la Kalobe zikishusha abiria.

Mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Maimuna Abdallah alisema kuwa aliliona Lori hilo lenye trela likishuka kwa mwendo wa kasi eneo la Nzovwe na baadaye likaigonga Hiace kwa nyuma ambayo ilipinduka upande wa kushoto kabla haijaigonga Hiace nyingine ambayo nayo ilipinduka.

Gazeti hili lilishuhudia majeruhi walioumia vinaya wakipatiwa huduma katika hospitali ya rufaa Mbeya na kulazwa ambapo watatu kati ya majeruhi hao wamelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi.

‘’Tumepokea majeruhi 11 wote hali zao ni mbaya wamelazwa katik wodi namba 1 na namba 2 watatu hali zao ni mbaya zaidi wako chini ya uangalizi maalumu,’’alisema Muuguzi mkuu wa Hospitali ya rufaa Mbeya Dkt. Thomas Isdory.

Aidha Dkt. Isdory alisema kuwa wamepokea mwili wa mtu mmoja mwanaume ambaye alikutwa na tiketi yenye jina la Joshua anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25-30.

Aliwataja majeruhi waliolazwa hospitalini hapo kuwa ni Said Omar, William Claud,Jesse Joseph, Eliah, Ambakisye, Josia Chonga, Godi Sanga, Nasra Nyagawa, Jane Mligo na wawili ambao bado majina yao hayajatambuliwa.

Post a Comment