Ads (728x90)


















TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” KUHUSIANA NA HALI YA UHALIFU KWA KIPINDI CHA KUANZIA JANUARI 2012 HADI DESEMBA TAREHE 30/12/2012.

1.0.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi DIWANI ATHUMANI anatoa shukrani na pongezi za dhati kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya kutokana na ushirikiano waliouonyesha kwa Jeshi la Polisi katika jukumu kubwa la kulinda usalama wa maisha na mali zao kwa  kipindi cha mwaka huu 2012 unaotarajia kumalizika leo. Ifuatayo ni taarifa fupi kuhusiana na  taswira ya hali ya uhalifu katika Mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha mwaka 2012.
1.1.Katika kipindi cha kuanzia 01.01.2012 hadi tarehe 30.12.2012  kwa ujumla hali ya uhalifu Mkoa wa Mbeya ilikuwa shwari. Hata hivyo pamoja na hali hiyo ya  ushwari kulikuwepo na baadhi ya matukio makubwa ya jinai mathalani  Mauaji,Unyang’anyi wa kutumia silaha,Unyang’anyi wa kutumia nguvu,Uvunjaji,kubaka, wizi wa Pikipiki wizi wa mifugo n.k. ambayo yaliweza kushughulikiwa na Jeshi la Polisi kwa mafanikio makubwa kwani watuhumiwa wameweza kukamatwa na kufikishwa Mahakamani na baadhi yao kesi zimemalizika na wengine  kesi zao zinaendelea kusikilizwa zikiwa katika hatua mbalimbali.
          [a] TATHMINI YA MAKOSA  YOTE YA JINAI.

Katika kipindi hicho cha Jan  – Desemba   2012 jumla ya makosa 29,849 yaliripotiwa katika vituo mbalimbali vya Polisi , wakati kipindi kama hicho mwaka 2011 makosa 25,699 yaliripotiwa, hivyo kuna ongezeko la makosa 4,150  sawa na asilimia 16. Ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa makosa madogo madogo kama vile kutumia lugha ya matusi,kutishia,shambulio,wizi n.k.
         [b] TASWIRA YA HALI YA UHALIFU YA MKOA.
Katika kipindi hicho cha Jan – Desemba  2012 jumla ya makosa 5,761 ambayo ni kero kwa jamii kati ya hayo makubwa  1,430  na madogo 4,331 yaliripotiwa , wakati kipindi kama hicho mwaka 2011 makosa 7,550 kati ya hayo  makubwa  1,479  na madogo  6,071 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu  la makosa 1,789  sawa na asilimia 23. Hata hivyo upungufu huo wa makosa makubwa unatokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali katika kupambana na uhalifu na

wahalifu hususani kwa makosa makubwa. [ Tazama kiambatanisho jedwali  A na  B]                                                                                                    
Hapa chini ni jedwali “A” kuonyesha mchanganuo wa makosa makubwa  ambayo ni kero kwa jamii yaliyoripotiwa kipindi cha Jan-Des 2012 ikilinganishwa na kipindi kama hichi mwaka 2011.                                                                                                             
JEDWALI  ‘A’
S/NO

MAKOSA
01.01.2012 HADI
30.11. 2012
01.01. 2011 HADI
30.12.2011
TOFAUTI
ASILIMIA
1
MAUAJI
276
354
-78
-22
2
KUBAKA
358
379
-21
-5
3
UNYANG’ANYI KATIKA BARABARA KUU
4
14
-10
-71
4
UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA
14
17
-3
-17
5
UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU
165
171
-6
-3
6
UVUNJAJI
266
292
-26
-8
7
WIZI WA MIFUGO
233
196
+37
+18
8
WIZI WA PIKIPIKI
114
56
+58
+103
9
WIZI
4, 860
6,071
-1.211
-19

JUMLA
5,761
7,550
-  1,789
-23

1.2. Pamoja na kupungua kwa makosa makubwa changamoto bado ipo kwa baadhi ya makosa kama vile WIZI WA PIKIPIKI na WIZI WA MIFUGO ambayo yameongezeka. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi DIWANI ATHUMANI, anawataka waendesha Pikipiki waendelee kuwa na umoja katika kudhibiti uhalifu na kutoa taarifa za uhalifu kwa mamlaka zinazohusika  hasa kwa watu ambao wanawatilia shaka.

                                                                                                                  
2.0.TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO NA JITIHADA  ZA  POLISI        
      KWA  KUSHIRIKIANA NA WANANCHI  NA WADAU MBALIMBALI.

Katika kipindi cha kuazia tarehe 01.01.2012 hadi tarehe 30.12.2012 makosa kadhaa yatokanayo na jitihada za Polisi na wadau wengine yalidhibitiwa  kwa mafanikio makubwa. Hii ni kutokana na misako,doria na operesheni mbalimbali zilizofanyika.                                                                                                          
Hapa chini ni jedwali  “B” kuonyesha mchanganuo wa makosa  yatokanayo na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana wananchi na wadau mbalimbali ambayo ni kero kwa jamii yaliyoripotiwa kipindi cha Jan-Des 2012 ikilinganishwa na kipindi kama hichi mwaka 2011.
 JEDWALI ‘B’
S/NO
        MAKOSA
01.01.2012 HADI 30.12.2012
01.01.2011 HADI 30.12. 2011.
TOFAUTI
ASILIMIA
                1
WAHAMIAJI HARAMU
72
24
+48
+200
2
KUPATIKANA NA BHANGI
171
148
+23
+15
  3
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
91
44
+47
+106
4
KUPATIKANA NA MTAMBO WA GONGO
12
4
+8
+200
 5
KUPATIKANA NA SILAHA
24
15
+9
+60
6
KUPATIKANA NA RISASI
10
3
+7
+233
7
MAGENDO
10
4
+6
+150
8
KUPATIKANA NA MADAWA YA KULEVYA.
6
-
+6
+600
9
KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
22
17
+5
+29

JUMLA

418
259
+159
+61
                                                                                                                                         
                                                                                                                                     
Kuongezeka kwa makosa haya kunatokana na jitihada za dhati za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine katika kukabiliana na uhalifu.                                                                                         
2.1 BAADHI YA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.
 Katika kipindi cha kuanzia tarehe 01.01.2012 hadi tarehe 30.12.2012 baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na :-                                                                                                                        
·        Pombe ya moshi [gongo] yenye ujazo wa lita 787 zilikamatwa pamoja na mitambo 12  ya kutengenezea pombe hiyo.   
·        Bhangi yenye uzito wa Kgm 942   na  gram 631 pamoja na shamba moja lenye ukubwa wa ekari 1 ilikamatwa.

·        Wahamiaji haramu  535 wamekamatwa katika mchanganuo ufuatavyo:-
Ø Ethiopia   192
Ø Somalia    298
Ø Kenya       1
Ø Malawi   11
Ø DRC      33
·        Silaha 20  zimekamatwa kati ya silaha hizo Gobole 16, SMG 2 na risasi 178, Riffle  1, S/gun 1 na  risasi 12.
·        Jumla ya watuhumiwa  9,581 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali kati yao 5,101 wamefikishwa Mahakamani.
·        Magari 11 yaliyokuwa yameibwa yamepatikana.
·        Noti bandia 292 kati ya hizo 197 @ tshs 10,000/= sawa na tshs 1,970,000/= na noti 95 @ tshs 2,000/= sawa na tshs 190,000/= zilikamatwa.
·        Madawa ya kulevya aina ya Cocaine Kgm 3 na gram 979 na Heroine gram 4.5 yalikamatwa.
·        Mafuta ya wizi aina ya Diesel lita 5,855 zilikamatwa.
·        Bidhaa za magendo za aina mbalimbali zenye thamani ya tshs 9,800,000/= zilikamatwa.
·        Mifuko 45 ya simenti maalum kwa ajili ya ujenzi  wa barabara ilikamatwa
·        Pikipiki 11 zilikamatwa katika matukio mbalimbali  ya kihalifu.











·        Milipuko ya aina mbalimbali kwa ajili ya kupasulia miamba /mawe yenye thamani USD 3,600  [tshs 5,760,000/=] iliyoporwa ilikamatwa ambayo ni :-
Ø Kubella pc 275
Ø Detector pc 309
Ø Cordetex Roll mita 1,750                                                          
Ø Led pc 7
Ø Trunkerline Roll 13.                                                                      
                                                                                                           
·        Kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu kama inavyoonekana kwenye jedwali “A”
                                                                                              
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi DIWANI ATHUMANI  pamoja na kutoa shukrani kwa mafanikio hayo, bado anaendelea kutoa rai kwa jamii kulipa ushirikiano wa karibu Jeshi la Polisi ili kuwafichua wahalifu kwani  uhalifu unarudisha nyuma maendeleo ya mwana Mbeya mmoja mmoja /familia hadi Mkoa mzima  na Taifa kwa ujumla.
3.0 MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
Makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani katika kipindi cha mwaka  2012 hususani ya ajali yamepungua  ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2011. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi DIWANI ATHUMANI  anasisitiza kuwa pamoja na upungufu huo wa matukio ya ajali  bado zipo changamoto katika kukabiliana na matukio ya ajali Mkoa wa Mbeya ambayo ni pamoja na :-
§  Mwendo kasi wa magari /Pikipiki kwa baadhi ya madereva na kutokuwa makini kuzingatia sheria za usalama barabarani na baadhi ya wananchi kushabikia mwendo kasi.                                                                                  
§  Ulevi
§  Kupita gari lingine bila tahadhali [Overtaking]
§  Tatizo la kimiundo mbinu kamamvile milima/maporomoko n.k
§  Mwendo kasi [Overspeed] maeneo ya tambarale.
§  Wananchi/watembea kwa miguu kutokuwa makini na matumizi ya barabara.






Hapa chini ni jedwali “C” kuonyesha mchanganuo wa makosa  ya ukiukwaji wa sheria za  usalama barabarani yaliyoripotiwa kipindi cha Jan-Des 2012 ikilinganishwa na kipindi kama hichi mwaka 2011.                                                                                                                                                                                     
JEDWALI  ‘C’
S/NO
        MAKOSA
01.01.2012 HADI 30.12.2012
01.01.2011 HADI 30.12. 2011.
TOFAUTI
ASILIMIA
                1
JUMLA YA MAKOSA YOTE YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
52,716
40,823
+11,893
+29
2
MATUKIO YA AJALI
598
686
- 88
-12
3
AJALI ZA VIFO
246
254
   -8
-3
4
WATU WALIOKUFA
315
320
-5
-1
 5
AJALI ZA MAJERUHI
352
432
-80
-18
6
WATU WALIOJERUHIWA
802
812
-10
-1
7.
TOZO [NOTIFICATION]
KUTOKA KWA WAKOSAJI MBALIMBALI.

1,250,790,000/=
802,130,000/=
+448,660,000/=
+55
 
4.0 HALI YA KISIASA / MIGOGORO YA KIJAMII NA DINI.
4.1 Hali ya kisiasa, Inaendelea vizuri ,vyama vya siasa Mkoani Mbeya ambavyo ni pamoja na  CCM,CHADEMA,CUF,TLP na NCCR- MAGEUZI, vimeendelea kufanya harakati zake kisiasa ikiwa ni pamoja na mikutano ya hadhara kwa usalama. Hata hivyo matukio kadhaa ya uvunjifu wa amani yaliripotiwa kutokea katika Kata za Kiwira Wilaya ya Rungwe na  Mpapa na Kamsamba  Wilayani Momba wakati wa kampeni za marudio ya uchaguzi mdogo wa nafasi za udiwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji , matukio hayo yaliweza kudhibitiwa kwa watuhumiwa kadhaa  kukamatwa na kufikishwa Mahakamani, kesi zao zinaendelea.    


                                                                                                                    
4.2. MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI.  
Katika kipindi hicho hakuna tukio kubwa  lililoripotiwa kutokea.
4.3 MASUALA YA IMANI ZA KIDINI.
Katika kipindi hicho hakuna tukio la uvunjifu wa amani lililohusiana na migogoro ya imani za kidini lililiripotiwa kutokea.                           
        CHANGAMOTO.
Miongoni mwa changamoto zilizojitokeza kwa kipindi hiki ni pamoja na :-..   
ü Baadhi ya wananchi kuendelea kuficha wahalifu na uhalifu katika maeneo yao na kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
ü Bado baadhi ya wananchama wa vyama/ viongozi wa siasa hawajaona umuhimu wa kutii sheria wao wenyewe na ama kuendelea kutoa maneno ya kuwagawa wana Mbeya.
                                              
5.0 HITIMISHO / WITO WA KAMANDA.
§  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejitahidi kudumisha utulivu na amani katika kipindi chote cha mwaka 2012 ikiwa ni pamoja na kudhibiti uvunjifu wa amani uliotaka kujitokeza kutokana na migogoro ya kijamii katika baadhi ya maeneo kama vile Vijiji vya Ntokela na Kiwira Wilaya ya Rungwe,Tunduma na  Kamsamba Wilaya ya Momba na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa Polisi Diwani Athumani anatoa wito kwa wakazi/wana Mbeya  kwa mwaka ujao wa 2013 :-
§  Kuendelea kutoa /kulipa ushirikiano wa karibu  Jeshi la Polisi katika kufichua na kupambana na uhalifu na wahalifu Mkoa wa Mbeya ili kuhakikisha uhalifu unazidi kupungua kama sio kumalizika kabisa na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kujipanga kuhakikisha Mkoa unakuwa shwari na wananchi wanaendelea kufanya shughuri zao za kujitafutia  maendeleo kwa amani,utulivu na usalama na pia inashiriki katika ulinzi na usalama wao wenyewe na mali zao.
§  Wananchi kuacha tabia ya kuchukua sheria mkononi katika matatizo                       yanayowakabili badala yake watafute ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo   /utaratibu unaokubalika kisheria  kupitia mamlaka husika yakiwemo  matatizo ya kijamii.



§  Kamanda ameeleza kuwa vitendo vya  kufunga barabara na kuchoma matairi ni uharibifu wa miundo mbinu inayopelekea hasara kubwa kwa Taifa na usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara. Aidha vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha  kuwa na watu ambao wameonyesha kutokuwa na nia njema ikiwa ni pamoja na kufanya uporaji                                                                                                  
§  Viongozi wote wa dini/siasa/jamii n.k waendelee  kuwafanya wana Mbeya kuwa wamoja badala ya kuwagawa bila kuathiri shughuli zao ziwe za kidini/kisiasa/kijamii wakikumbuka kuwa umoja ndio chachu kubwa ya maendeleo.                                                                                                                    
§  Aidha  anawatakia wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya  na watanzania kheri ya mwaka   mpya 2013. Aidha Kamanda anasisitiza  kusherehekea kwa amani na utulivu pasipo kuhusisha vitendo vya vurugu,uchomaji moto matairi , kufunga barabara na uendeshaji mbovu wa vyombo vya moto kwani ni kinyume cha sheria.

Signed By
[ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

                                                                                                     
























Post a Comment