Pichani Shule zetu - Usafi chooni inashindikana?

Choo cha shule ya msingi Lipangala, huko sehemu mojawapo ya Ludewa. Nashangaa hata kusafisha eneo linalozunguka choo ni:
- Mbunge achangie?
- Serikali ipangie bajeti?
- Wazazi wachangie?
- Walimu wahimizwe?
- Kaka Mkuu na Dada Mkuu wa shule hawana akili timamu?
- Elimu ya maisha na kujitegemea mashuleni imesitishwa?
​Kama mambo hayo hayahitajiki kwa nini kusiwe na taratibu za wanafunzi kufanya usafi wa mazingira yao? Nahofia hapa ipo siku nyoka atakanyagwa mkia kisha kumng'ata mguu mwanafunzi.(source jamiiforums)
Post a Comment