Ads (728x90)



Image copyrightBoko Haram
Image captionPicha hizo zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama (Government Technical College Bama (GTCB)
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram wamezindua kiwanda wanachotumia kuunda mabomu na silaha zingine kali Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Image copyrightBoko Haram
Image captionPicha hizo zilitumwa kwa idhaa ya Hausa ya BBC kupitia kwa namba iliyosajiliwa nchini Cameroon.
Kupitia kwa mtandao wa WhatsApp picha hizo zilitumwa kwa idhaa ya Hausa ya BBC kupitia kwa namba iliyosajiliwa nchini Cameroon.
Image copyrightContributor
Image captionWapiganaji hao wakipaka rangi silaha zao
Picha hizo zinaonesha watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi hilo wakiwa kwenye karakana fulani wakitengeneza silaha zenye uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa.
Picha hizo zinaaminika kuwa zilipigwa katika jimbo la Borno nchini Nigeria.
Image copyrightBoko Haram
Image captionMhandisi wa Boko Haram akiunda silaha
Wachunguzi wanasema kuwa picha hizo zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama (Government Technical College Bama (GTCB).
Haijabainika iwapo mashine hizo za chuo hicho anuai zilinaswa na maafisa wa jeshi la Nigeria au la.
Image copyrightBoko Haram
Image captionSehemu ya silaha zilizoundwa na Boko Haram
Hata hivyo Bama ni moja ya miji iliyokombolewa na jeshi la Nigeria.
Image copyrightBoko Haram
Image captionSehemu ya kwanza ya mifereji ikikatwa kutengeneza silaha
Licha ya waasi hao kupigwa na kuondolewa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa Nigeria kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi ambayo yamewaacha wa Nigeria wengi wakishangaa wanakotoa silaha hizo kali.
Image copyrightBoko Haram
Image captionHuu ndio ushahidi wa kwanza kuwa kundi hilo linauwezo wa kutengeneza silaha kali.
Huu ndio ushahidi wa kwanza kuwa kundi hilo linauwezo wa kutengeneza silaha kali.(CHANZO BBC.COM)

Post a Comment