Ads (728x90)

Wanamichezo kutoka kikundi cha Tanzania Streets Workout cha Jijini Dar es salaam pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) Ulimboka Mwakilili wakiangalia mandhari ya bonde la Usangu kutokea juu upande wa wilaya ya Chunya kwenye eneo maarufu Viewing Area ambalo ni maalum kwa ajili ya utalii wa maparachuti

Hali ya hewa ya mvua, baridi na ukungu haikuwazuia kuendelea kufanya mazoezi ili kujenga afya na akili


Tanzania Streets Workout walipata fursa ya kutembelea kwenye eneo la Juu zaidi la barabara kutoka usawa wa bahari nchini ambalo lipo barabara ya Chunya hapo walipata fursa ya kuweka kibao chenye majina yao kama ishara ya alama na kuenzi utalii kwa kuwa eneo hilo ni la kipekee nchini 

Kiongozi wa wanamichezo kutoka Tanzania Streets Workouts Zola D King akizungumza na baadhi ya vijana alipotembelea kwenye shule ya Sekondari ya Iyunga ambayo hivi karibuni ilifikwa na janga la kuungua moto, hapo walipata fursa ya kufanya kazi za kuchekecha mchanga kwa ajili ya kufyatulia tofali za ujenzi wa mabweni ya shule hiyo.

Mandhari ya juu eneo la Chunya 

Msanii Ommy Lax akionesha mitindo mbalimbali ya mazoezi akiwahamasisha vijana kujihusisha na mazoezi alipotembelea shule ya sekondari Iyunga akiwa na kundi la Tanzania Streets Workout pamoja na waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji TAJATI

Baadhi ya waandishi wa Habari wa TAJATI wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa vyombo vya habari na wasanii wanamichezo  Tanzania Streets Work Out kwenye stendi ya Mabasi ya Nane Nane

Zola D King na Mwarabu Fighter wakishiriki matembezi ya hiari kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi,kutembelea vivutio vya ndani na kufanya usafi





 




Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyerembe Munassa akishiriki matembezi ya hiari yaliyoandaliwa na wanamichezo Tanzania Streets Workout na Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) matembezi hayo ya km 12  yalianzia ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya hadi Stendi Nane Nane Uyole

Safari inaendelea





Wakiendelea kukatisha mitaa ya Jiji la MBEYA kuhamasisha kufanya mazoezi, kutembelea utalii wa ndani na kufanya usafi wa mazingira

 








Msafara unaendelea haaooo wakikatisha mitaa kuwahamasisha wananchi kufanya usafi, kufanya mazoezi na kutembelea vivutio vya utalii







Mchaka!! mchaka Chinjaa!!! ndivyo ilivyokuwa kwa wanahabari wa TAJATI, Mkuu wa wilaya, wadau na Tanzania Streets workout








Mwendo Mdundo bila kuchoka safari ianendelea











Msafara uliowahusisha wanahabari wa TAJATI, wadau, Tanzania Streets Workout na mkuu wa wilaya ya Mbeya uliendelea



Katika maeneo mengine msafara ulilazimika kusimama na kusaidiana na wananchi kufanya usafi kama inavyoonekana pichani














Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyerembe Munassa akishiriki katika usafishaji wa mitaro eneo la Mwanjelwa akiwa ameambatana na wanahabari wa TAJATI na wasanii wanamichezo Tanzania Streets Workout









 




  














Kama ilivyo ada katika eneo la Kabwe Mkuu wa wilaya Mbeya Nyerembe Munassa akashiriki katika kufanya usafi karibu na dampo lililopo eneo hilo




















 
















Msafara huu ulichombezwa na hamasa kwa wananchi kujitokeza kufanya mazoezi wka kupiga Push Up barabarani




 


 



Post a Comment