Ads (728x90)

SAKATA LA MABWENI YALIYOTEKETEA IYUNGA SEKONDARI
-RC Amos Makalla ajipanga kwenda kutumbua majipu April 4
SAA chache baada ya kuweka post juu ya skendo inayohusu harambee ya uchangiaji kwa ajili ya mabweni ya Iyunga iliyobeba kichwa cha ‪#‎Amos‬Makalla akaribishwa Mbeya kwa Skendo" mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ameonesha umahiri mkubwa wa ufuatiliaji STORIES kwenye social network.
Mheshimiwa Makalla aliibuka na kueleza yaliyo moyoni mwake na kufafanua kuwa atafuatilia suala hilo na amepanga ratiba kwa ajili ya kutumbua jipu hilo April 4.
‘’Nimefuatilia kwa umakini hoja juu ya sakata hili, tarehe 4 nimepanga kufanya ziara Iyunga Sekondari,nitaenda kutumbua jipu huko,’’amesema Mheshimiwa Makalla akijibu post iliyoiwekwa mchana juu ya kile kinachoonekana ni matumizi mabaya ya fedha kwa harambee ambayo imeshindwa kufanyika. Awali kwenye page ya FB ya Rashid Mkwinda kulikuwa na post iliyohusu.....

Picha hizi ya mtandaoni inaonesha kuteketea kwa mabweni na namna ambavyo wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga walivyo mara baada ya nabweni yao kuteketea kwa moto

Ubungo Plaza eneo ambalo kulipanga kufanyika harambee kwa ajili ya uchangiaji wa Mabweni ya shule ya sekondari Iytunga Machi 19 ambayo iliahirishwa ghafla



Mkuu mpya wa mkoa wa Mbeya Amos Gabriel Makalla akikabidhiwa kitabu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abbas Kandoro

KUTEKETEA KWA MABWENI SEKONDARI IYUNGA
Amos Makalla akaribishwa Mbeya na SKENDO
-Mamilioni yadaiwa kutafunwa
-Harambee iliyopangwa kufanyika UBUNGO PLAZA yaahirishwa ghafla,
-Kamati ya fedha Mipango na Uchumi yaelezwa ilihamia Dar kwa ajili ya maandalizi, gharama za kukaa hotelini, kusafirisha,watendaji wa halmashauri ya Jiji, waandishi wa habari kutoka Mbeya zahojiwa.
-Wadau wahoji sababu ya harambee hiyo kuhamishiwa Dar badala ya Mbeya kwenye Ukumbi wa Mkapa unaomilikiwa na Jiji la Mbeya......KAA HAPO HAPO ITAKUJIA YOTE kupitia www.mkwinda.blogspot.com.. INAENDELEA KUFANYIWA UCHOKONOZI

Post a Comment