Ads (728x90)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa na wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni

Mkuu mpya wa wilaya ya Chunya Rehema Manase akila kiapo cha utii mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla

  

Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia Undalusyege Kitta akitia saini kwenye fomu ya kiapo mara baada ya kula kiapo cha utii na utumishi wa serikali mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chalya Julius Nyangindu akila kiapo cha utii serikalini mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akila kiapo cha utii serikalini mbele ya aMkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
 

Mkuu wa wilaya ya Mbarali Reuben Ndiza Mfune akitia saini kwenye fomu ya kiapo baada ya kula kiapo cha utii na utumishi serikalini mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla


MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka wakuu wapya wa wilaya kuifanya serikali kuwa rafiki na wananchi ili kusaidia kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii kwenye maeneo yao.
Makalla aliyasema hayo wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Mbeya ambao waliteuliwa hivi karibuni na Rais John Pombe Magufuli.
‘’Falsafa yangu ni kuwa na serikali rafiki na wananchi,Ofisi za serikali ziwe kimbilio la wananchi, msizifanye za serikali kuwa kama kituo cha polisi,’’alisema Makalla.
Alisema katika utendaji wake amekuwa na desturi ya kuwafuata wananchi na kusikiliza matatizo yao ambapo amewataka wakuu hao wa wilaya nao waendelezea desturi hiyo ambayo ndiyo inayosaidia uwajibikaji wa serikali  kwa wananchi wake.
‘’Wananchi wanazo kero nyingi, kusikiliza kero za wananchi ndio kipimo chenu cha uwajibikaji, kasikilizeni kero za wananchi zile zitakazowashinda zileteni kwangu kwa maandishi zinifikie Jumatatu asubuhi,’’alifafanua.
Alisema si vyema kuwaacha wananchi wabaki na manung’uniko kwa kuwa kufanya hivyo kunawajengea chuki na serikali yao na hivyo kupunguza uwajibikaji na kasi ya maendeleo ya wananchi.
Aidha Makalla ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya aliliagiza Jeshi la Polisi kupambana vikali na majambazi wanaotumia silaha kwa kuwa hao wamekuwa wakiwajengea hofu na hata kuwaua raia wasio na hatia.
‘’Polisi nawaagiza jambazi akija na moto na wewe na wewe nenda kwa moto,nendeni mkapambane na majambazi, mjue kuwa jambazi mwenye silaha akikuwahi amekuua, hivyo ili asiwahi kukuua muanze yeye hili litasaidia kuwamaliza majambazi,’’alisisitiza Makalla.
Wakuu wa wilaya walioapishwa na wilaya zao kwenye mabano ni pamoja na Rehema Manase Madusa(Chunya),Claudia Undalusyege Kitta(Kyela)Chalya Julius Nyangindu(Rungwe)Reuben Ndiza Mfune(Mbarali) na William Paul Ntinika(Mbeya).

Post a Comment