Ads (728x90)


Prof Lipumba akiteta jambo na aliyekuwa Mgombea Urais kwa vyama vinavyounga UKAWA Edward Lowassa
 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa OAU Dkt Salim Ahmed Salim


a
Prof Lipumba,(CUF) Dkt Slaa(CHADEMA) na Mwigulu Nchemba(CCM) mara baada ya viongozi hao kutangaza kuondoka kwenye vyama vyao

Dkt Slaa na Prof Lipumba mara baada ya kujiuzulu nyadhifa zao kwenye vyama vyao

Maalim Seif na aliyekuwa Mgombea Urais wa vyama vya UKAWA Edward Lowassa

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
-Aeleza sababu za kujiuzulu
-Adai aliwahi kumfuata Dkt Salim kugombea CUF akakataa
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye aliandika barua ya kujiuzulu Profesa Ibrahimu Lipumba ameibuka  na kubainisha kuwa aliwahi kumfuata aliyekuwa Katibu Mkuu wa OAU Dkta Salim Ahmed Salim ili agombee urais wa CUF lakini akakataa kwa kuwa yeye alikuwa ni mwanachama mwaminifu wa CCM.
Profesa Lipumba aliyasema hayo katika mahojiano maalum aliyofanya kupitia kipindi cha Power Breakfast kilichokuwa kikirushwa na Redio Clouds Fm jana asubuhi alipokuwa akielezea sababu za yeye kuandika barua ya kujiuzulu na dhamira yake ya kurejea katika chama hicho.
Alisema kuwa mwaka 2005 mara baada ya CCM kumbwaga Dkt Salim alimfuata ili agombee Urais kupitia CUF na kuwa Dkt. Salim alikataa akisema kuwa yeye ni mwanachama wa CCM na hawezi kukihama chama hicho na kujiunga na CUF.
Profesa Lipumba alisema hayo baada ya kuulizwa sababu za yeye kuendelea kuwa Mwenyekiti na kuwa  amekuwa akigombea urais bila kuwapisha wengine ndani ya chama ambapo alijibu kuwa yeye amekuwa akifanya jitihada za kuwatafuta watu wengine wagombee nafasi hiyo bila mafanikio na kuwa wazee wa chama wamekuwa wakimshinikiza aendelee kugombea nafasi hiyo.
 Aidha Prof Lipumba alibainisha kuwa Katibu Mkuu wake Maalim Seif Sharif Hamad amekuwa akikisaliti chama hicho kwa nia  kukiua  upande wa bara na hasa ndio sababu iliyomfanya yeye aamue kuandika barua ya kujiuzulu uenyekiti.
Alisema kuwa Maalim Seif alimgeuka na kufanya mazungumzo na CHADEMA kuhusu masuala ya Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) bila kumshirikishwa  ilhali yeye kama Mwenyekiti ndiye aliyepaswa kushiriki mazungumzo hayo na kufanya makubaliano juu ya mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Alibainisha kuwa kilichotokea kati yake na Maalim Seif ni usaliti kama ulivyotokea wakati wa Mzee Aboud Jumbe mwaka 1984, wakati  mazungumzo yakiendelea mmoja wa watu alifanya usaliti ambapo siri za vikao azipeleka kwa Mwalimu Nyerere hatimaye Mzee Jumbe akaamua kujiuzulu.
‘’Katibu Mkuu wangu alinigeuka, pamoja na kuwa mimi ndiye nilikuwa nashiriki vikao, yeye alikuwa akifanya vikao visivyo rasmi, kulikuwa na hujuma kwa bahati mbaya ama makusudi, alifanya mazungumzo na viongozi wa CHADEMA wenzetu wa CHADEMA wakatumia mwanya huo kutudhoofisha,’’alisema.
Prof Lipumba ambaye alikuwa akiulizwa maswali na wasikilizaji kupitia ujumbe mfupi wa simu na kuchagizwa maswali hayo na watangazaji waliokuwa wakikiongoza kipindi hicho Masoud Ali ‘Kipanya’ na Babra Hassan alisema kuwa ujio wa Edward Lowassa ni moja ya sababu zilizomfanya aandike barua ya kujiuzulu.
Akielezea sababu za kukosa subira na hivyo kulazimika kuandika barua ya kujiuzuliu alisema kuwa alishindwa kuvumilia kutokana na yeye kwamba atalazimika kuwa mpiga debe wa Lowassa ilhali anajuwa wazi mgombea huyo alikuwa amegubikwa na tuhuma za kukosa maadili ya uongozi.
Akijibu swali kama upo uthibitisho wa Lowassa kuhusika na tuhuma anazokabiliwa zinazoweza kumfikisha mahakamani Prof Lipumba alijibu kuwa Hayati Mwalimu Nyerere alishawahi kusema kuwa kijana huyu (Lowassa) ana mali zisizoelezeka hivyo ilitosha kumuona kuwa ana tuhuma za kujibu juu ya mali zake.
Hata hivyo alisema kuwa anaamini kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF kwa kuwa hakuna kikao kilichoketi kujadili barua yake na kukubaliwa kujiuzulu kwake na kuwa hata hivyo watu wengi walifika kumuomba arejee kwenye nafasi yake.
‘’Watu wengi walikuja kuniomba nirejee nikaamua kuandika barua ya kutengua barua yangu ya kujiuzulu nikajipangia hadi siku ya kuingia ofisini kuanza kazi , Katibu Mkuu akaniandikia barua kwamba nisirejee ofisini hadi atakaposhauriana na wanasheria wa chama,’’ alifafanua.
‘’Ibara ya 117 ya Katiba inasema kujiuzulu kutakamilika iwapo mamlaka iliyomchagua itakapokubali mamlaka iliyonichagua haikukutana hadi Mkutano mkuu hivyo kutengua kuliendelea kunifanya niendelee kuwa Mwenyekiti kabla maamuzi ya mkutano mkuu hayajapitishwa,’’alisisisiza.
Prof Lipumba pia alisema kuwa hana mpango wa kuanzisha chama chochote wala kujiunga na chama kingine na kuwa hawezi kuruhusu Lowassa aingie ndani ya CUF na kuwa kitendo cha Maalim Seif kutopeana mkono na Dkt Shein alifanya makosa na kuwa si kitendo cha uungwana.
Kadhalika alibainisha kuwa pamoja na tofauti zao za kisiasa kati yake na Maalim Seif walikutana naye Hospitali ya Hindu Mandar ambako walikutana na kupeana mikono pamoja na yeye kumfukuza kwenye chama.

Post a Comment

  1. PROMO DELIMA
    poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

    Bonus yang kami sediakan :
    * TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
    * Bonus referal sebesar 10%

    Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
    Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
    Come join and be a winer with us !!

    Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
    Livechat_____: delimapoker
    BBM__________: 7B960959
    Facebook_____: Facebook
    Phone number_: +85595678845

    ReplyDelete