Ads (728x90)

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu Jijini Mbeya wakiwa katika ibada ya swala ya Eid El Haj kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.


Ustadh idd Omar Pembe akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria ibada ya swala ya Eid El Haj uwanja wa sokoine leo asubuhi.


Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Mbeya wametakiwa kudumisha Umoja na Mshikamano miongoni mwao ili kujenga amani na utulivu katika dini.
Akizungumza wakati wa hutuba ya ibada ya swala ya Eid El Haj iliyoswaliwa kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, Ustadhi Idd Omar Pembe alisema kukosekana kwa mshikamano ndio chanzo cha kukosekana kwa amani na utulivu.

Ustadhi Pembe alisema dhana ya ubaguzi na kubaguana na kila mmoja kujifanyia lake kwa waislamu kunajenga chuki na uhasama hivyo ni vyema waislamu wakashikamana na kushirikiana kwa shida na raha hasa katika kipindi cha majanga.

Alisema ushirikiano na mshikamano unajenga mapenzi na kwamba Mwenyezi Mungu anawachukia watu wanaofarakana kwa kuwa kitendo hicho ni tabia ya shetani inayompeleka mtu motoni.

Awali akizungumza dhana ya ibada ya Eid El Haj Imamu wa msikiti Baraa Bin Azb Isanga Shekhe Ibrahim Bombo alisema kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wanaungana na waislamu wenzao duniani ambao wako katika ibada ya Hija huko Mecca Saudi Arabia.

Alisema Hija ni nguzo ya tano katika nguzo za Uislamu ambapo Mwislamu mwenye uwezo anapaswa kutekeleza ibada hiyo kwa mwaka mara moja katika maisha yake ikiwa ni pamoja na kutoa sadaka ya kuchinja mnyama kufuata mwenendo wa Nabii Ibrahimu.

Aidha Sheikh Ibrahimu alionya waislamu kutofanya maovu siku ya Idd kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kufanya madhambi siku ya kiyama.Waislamu Jijini Mbeya wameungana na waislamu wenzao kote duniani katika kusherehekea Eid El Haj na kuswali pamoja kwenye viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Post a Comment

 1. PROMO DELIMA
  poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

  Bonus yang kami sediakan :
  * TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
  * Bonus referal sebesar 10%

  Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
  Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
  Come join and be a winer with us !!

  Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
  Livechat_____: delimapoker
  BBM__________: 7B960959
  Facebook_____: Facebook
  Phone number_: +85595678845

  ReplyDelete