Prof Lipumba akiteta jambo na aliyekuwa Mgombea Urais kwa vyama vinavyounga UKAWA Edward Lowassa |
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa OAU Dkt Salim Ahmed Salim |
a |
Prof Lipumba,(CUF) Dkt Slaa(CHADEMA) na Mwigulu Nchemba(CCM) mara baada ya viongozi hao kutangaza kuondoka kwenye vyama vyao |
Dkt Slaa na Prof Lipumba mara baada ya kujiuzulu nyadhifa zao kwenye vyama vyao |
Maalim Seif na aliyekuwa Mgombea Urais wa vyama vya UKAWA Edward Lowassa |
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad |
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe |
-Aeleza
sababu za kujiuzulu
-Adai
aliwahi kumfuata Dkt Salim kugombea CUF akakataa
Aliyewahi
kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye aliandika barua ya kujiuzulu
Profesa Ibrahimu Lipumba ameibuka na kubainisha
kuwa aliwahi kumfuata aliyekuwa Katibu Mkuu wa OAU Dkta Salim Ahmed Salim ili
agombee urais wa CUF lakini akakataa kwa kuwa yeye alikuwa ni mwanachama
mwaminifu wa CCM.
Profesa
Lipumba aliyasema hayo katika mahojiano maalum aliyofanya kupitia kipindi cha
Power Breakfast kilichokuwa kikirushwa na Redio Clouds Fm jana asubuhi alipokuwa
akielezea sababu za yeye kuandika barua ya kujiuzulu na dhamira yake ya kurejea
katika chama hicho.
Alisema kuwa
mwaka 2005 mara baada ya CCM kumbwaga Dkt Salim alimfuata ili agombee Urais
kupitia CUF na kuwa Dkt. Salim alikataa akisema kuwa yeye ni mwanachama wa CCM
na hawezi kukihama chama hicho na kujiunga na CUF.
Profesa
Lipumba alisema hayo baada ya kuulizwa sababu za yeye kuendelea kuwa Mwenyekiti
na kuwa amekuwa akigombea urais bila
kuwapisha wengine ndani ya chama ambapo alijibu kuwa yeye amekuwa akifanya
jitihada za kuwatafuta watu wengine wagombee nafasi hiyo bila mafanikio na kuwa
wazee wa chama wamekuwa wakimshinikiza aendelee kugombea nafasi hiyo.
Aidha Prof Lipumba alibainisha kuwa Katibu
Mkuu wake Maalim Seif Sharif Hamad amekuwa akikisaliti chama hicho kwa nia kukiua upande wa bara na hasa ndio sababu iliyomfanya
yeye aamue kuandika barua ya kujiuzulu uenyekiti.
Alisema kuwa
Maalim Seif alimgeuka na kufanya mazungumzo na CHADEMA kuhusu masuala ya Umoja
wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) bila kumshirikishwa ilhali yeye kama Mwenyekiti ndiye aliyepaswa
kushiriki mazungumzo hayo na kufanya makubaliano juu ya mchakato wa kuelekea
uchaguzi mkuu 2015.
Alibainisha
kuwa kilichotokea kati yake na Maalim Seif ni usaliti kama ulivyotokea wakati
wa Mzee Aboud Jumbe mwaka 1984, wakati
mazungumzo yakiendelea mmoja wa watu alifanya usaliti ambapo siri za
vikao azipeleka kwa Mwalimu Nyerere hatimaye Mzee Jumbe akaamua kujiuzulu.
‘’Katibu
Mkuu wangu alinigeuka, pamoja na kuwa mimi ndiye nilikuwa nashiriki vikao, yeye
alikuwa akifanya vikao visivyo rasmi, kulikuwa na hujuma kwa bahati mbaya ama
makusudi, alifanya mazungumzo na viongozi wa CHADEMA wenzetu wa CHADEMA wakatumia
mwanya huo kutudhoofisha,’’alisema.
Prof Lipumba
ambaye alikuwa akiulizwa maswali na wasikilizaji kupitia ujumbe mfupi wa simu
na kuchagizwa maswali hayo na watangazaji waliokuwa wakikiongoza kipindi hicho
Masoud Ali ‘Kipanya’ na Babra Hassan alisema kuwa ujio wa Edward Lowassa ni
moja ya sababu zilizomfanya aandike barua ya kujiuzulu.
Akielezea
sababu za kukosa subira na hivyo kulazimika kuandika barua ya kujiuzuliu
alisema kuwa alishindwa kuvumilia kutokana na yeye kwamba atalazimika kuwa
mpiga debe wa Lowassa ilhali anajuwa wazi mgombea huyo alikuwa amegubikwa na
tuhuma za kukosa maadili ya uongozi.
Akijibu
swali kama upo uthibitisho wa Lowassa kuhusika na tuhuma anazokabiliwa
zinazoweza kumfikisha mahakamani Prof Lipumba alijibu kuwa Hayati Mwalimu Nyerere
alishawahi kusema kuwa kijana huyu (Lowassa) ana mali zisizoelezeka hivyo ilitosha
kumuona kuwa ana tuhuma za kujibu juu ya mali zake.
Hata hivyo
alisema kuwa anaamini kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF kwa kuwa
hakuna kikao kilichoketi kujadili barua yake na kukubaliwa kujiuzulu kwake na
kuwa hata hivyo watu wengi walifika kumuomba arejee kwenye nafasi yake.
‘’Watu wengi
walikuja kuniomba nirejee nikaamua kuandika barua ya kutengua barua yangu ya
kujiuzulu nikajipangia hadi siku ya kuingia ofisini kuanza kazi , Katibu Mkuu
akaniandikia barua kwamba nisirejee ofisini hadi atakaposhauriana na wanasheria
wa chama,’’ alifafanua.
‘’Ibara ya
117 ya Katiba inasema kujiuzulu kutakamilika iwapo mamlaka iliyomchagua
itakapokubali mamlaka iliyonichagua haikukutana hadi Mkutano mkuu hivyo
kutengua kuliendelea kunifanya niendelee kuwa Mwenyekiti kabla maamuzi ya
mkutano mkuu hayajapitishwa,’’alisisisiza.
Prof Lipumba
pia alisema kuwa hana mpango wa kuanzisha chama chochote wala kujiunga na chama
kingine na kuwa hawezi kuruhusu Lowassa aingie ndani ya CUF na kuwa kitendo cha
Maalim Seif kutopeana mkono na Dkt Shein alifanya makosa na kuwa si kitendo cha
uungwana.
Kadhalika
alibainisha kuwa pamoja na tofauti zao za kisiasa kati yake na Maalim Seif
walikutana naye Hospitali ya Hindu Mandar ambako walikutana na kupeana mikono
pamoja na yeye kumfukuza kwenye chama.
PROMO DELIMA
ReplyDeletepoker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya
Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%
Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!
Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845