Baadhi ya vyakula na nguo ziliztolewa na wanafunzi, wafanyakazi na marafiki wa chuo kikuu cha Mzumbe Campus ya Mzumbe kwa watoto yatima wa Huruma Simike Jijini Mbeya. |
Jengo la Utawala Chuo Kikuu cha Mzumbe Campus ya Mbeya |
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Campus ya Mbeya Profesa Kihanga akiwa na baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Simike Jijini Mbeya. |
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Campus ya Mbeya wakiwa katika kituo cha watoto yatima Simike |
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Campus ya Mbeya Profesa Kihanga akiwa na mmoja wa watoto wadogo wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima Simike Mbeya. |
Baadhi ya wanafunzi wa chuo Kikuu cha Mzumbe Camous ya Mbeya |
Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Huruma Simike Jijini Mbeya Anna Kasile akitoa maelezo juu ya kituo hicho |
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiwa na baadhi ya misaada waliyoiwakilisha kwa kituo cha watoto yatima Simike. |
WANAZUONI wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Campus ya Mbeya leo mchana wameungana na Watanzania katika kusherehekea siku ya Muungano kwa kutoa misaada ya kijamii kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Malezi Ya Huruma kilichopo Simike Jijini Mbeya.
Msaada huo wa nguo, vyakula, sabuni na mafuta pamoja na fedha taslimu vyenye thamani ya Sh. milioni 3 zimetokana na michango ya Wafanyakazi wa Chuo hicho ikiwa ni pamoja na walimu na wanafunzi na baadhi ya marafiki ambao walilenga kuuungana na watoto yatima katika kudumisha umoja, undugu na mshikamano pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Chuo hicho Profesa Ernest Kihanga alisema kuwa, walipata wazo hilo na kuona umuhimu wa kuihusisha hiyo muhimu kwa Taifa la Tanzania kwa kuishirikisha jamii ya watu wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuona umuhimu wa kuwatembelea watoto wanaolelewa katika kituo hicho kutoa walichonacho.
Profesa Kihanga alisema siku hiyo imekuwa ni muhimu kwa Tanzania kutokana na historia yake kwa kutimiza miaka 50 ya Muungano ambapo ndani yake kulikuwa na changamoto nyingi zikiwemo matatizo mbalimbali ya kijamii na kwamba kwa kushirikiana na watoto yatima kutajenga historia yenye kumbukumbu kubwa kwa watoto hao juu ya Muungano wa nchi zetu.
''Hii itabaki kichwani mwa watoto hao, watakumbuka siku muhimu ya leo iliyoambatana na misaada tuliyotoa kwao'' alisema.
Naye Mhadhiri Msaidizi wa chuo hicho John Stephen alisema kuwa,walimu pamoja na wanafunzi wa chuo hicho waliketi chini na kuona umuhimu wa kuungana na watu wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kufurahia kwa pamoja siku hiyo.
''Sisi ni sehemu ya jamii, tunaungana na watoto hawa ili nao wajione ni sehemu ya jamii inayofurahia siku hiina wengine bila kujali tofauti ya maisha baina ya kundi moja na jingine''alisema Stephen ambaye pia ni Mwanasheria na wakili wa kujitegemea.
Kwa upande wake Neema Mwalyagile ambaye pia ni mhadhiri Msaidizi wa Chuo hicho alisema kuwa watu wa jinsia na maisha tofauti wanayo fursa ya kujua historia ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na kwamba kwa kutumia siku hii muhimu watoto hao watabaki na kumbukumbu hiyo kwa miaka mingi.
Ladislaus Rwekaza ni Mhadhiri Msaidizi chuoni hapo ambaye pia alitoa wito kwa jamii kuona umuhimu wa kuenzi siku hiyo ya Muungano kwa kufanya mambo ya kijamii ambapo Waziri wa Afya wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho Gift Segumba aliitaka jamii na taasisi za serikali na binafsi kuona umuhimu wa kuisadia jamii ya watu wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Akizungumza wakati akipokea msaada huo Mlezi wa Kituo cha Huruma cha Simike chenye jumla ya watoto 120 Anna Kasile alisema kuwa amepokea msaada huo kwa wakati muafaka ambapo kuna baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari Sumbawanga ambao wanalelewa na kituo hicho walirejeshwa kutokana na kukosa karo ya kuwalipia.
Alisema anakumbana na changamoto nyingi za uendeshaji wa kituo hicho na kwamba hata hivyo wanajamii hususani wanafunzi wa vyuo vilivyopo Jijini Mbeya wamekuwa wakijitokeza mara kwa mara kusaidia kwa namna moja ama nyingine kwa kutoa misaada ya hali na mali.
''Watoto hawa wanalelewa na Mungu mwenyewe, kuna wakati huwa tunafikiria siku hiyo tutakula nini lakini kwa miujiza hutokea wasamaria wema na kutoa misaada ya nguo, vyakula, sabuni, vifaa vya masomo na fedha,''
Alisema kuwa mtoto mdogo katika kituo hicho ana umri wa miezi minne ambaye alipatikana kwa kuokotwa na mkubwa kabisa ni mwanafunzi aliyeko chuo kikuu ambapo baadhi yao waliopitia kituoni hapo ni watumishi wa serikali.
Post a Comment