Na Kibada Kibada –Katavi.
Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi
Selemani Kakoso ametoa misaada ya mbalimbali ya kijamii katika kuinua
elimu jimboni ikiwa ni pamoja na kugawa computer Mpakato ‘laptop’ kwa shule
zote za sekondari zilizoko kwenye jimbo lake.
Kakoso pia amesaidia vitabu vya masomo ya sekondari kwa shule
za Sekondari Karema,Mpanda Ndogo Sekondari pamoja na kusaidia madawati
600 kwa shule zote za msingi 50 katika jimbo hilo katika kukabiliana na
changamoto za madawati zinazoikabili shule nyingi za sekondari katika mkoa wa
Katavi.
Shule zilizonufaika na Kompyuta
Mpakato ni pamoja na Shule ya wazazi ya Milala,Karema,Kabungu,Mpandandogo,Ilandamilumba,Mwese,Karema.Ikola,na
Mishamo ambazo zimo katika jimbo lake mbali ya kutoa Kompyuta hizo pia alisaidia
kuweka umeme wa jua kwa kutumia mfuko wa jimbo kwenye sekondari hizo na
zahanati ili kuhakikisha masomo yanatolewa kwa nyakatio zote.
Pamoja na msaada huo amewagawia
vijana jezi na mipira ili kuendeleza sekta ya michezo katika jimbo hilo ikiwa
ni pamoja na kutoa elimu kwa vijana wa kike na kiume kuunda vikundi vya
uzalishaji mali kwenye Mashina ya Wakereketwa na kuwawezesha mitaji kwa kila Shina
kiasi cha shilingi 500,000 ili waweze kuanzisha miradi ya uzalishaji mali
waweze kujitegemea.
Aidha Walimu wa kila shule kati ya 50
katika jimbo hilo amewawezesha kwa kuwapa mtaji wa shilling laki moja moja ili
kuanzisha miradi ya uzalishaji kwenye shule zao ili kupunguza ukali wa maisha kutokana
na walimu hao kutegemea mishahara pekee kukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Post a Comment