Jenister Mhagama |
Baadhi ya Wanafunzi wa shule moja ya Sekondari Nchini.(Picha kwa hisani ya Mtandao) |
Na
Kibada Kibada –Katavi,
IMEEELZWA
kuwa serikali bado haijaweka sera kwa wanafunzi wanaopata ujauzito mashuleni
kurejea kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Hayo
yamebainika katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda hivi karibuni na Kaimu Ofisa Elimu wa Sekondari Stephen Masungwa
akifafanua hoja iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima kutaka
wanafunzi wanaopata ujauzito kurejea mashuleni.
‘’Hadi
sasa hakauna sheria inayoruhusu wanafunzi waliopata ujauzito mashuleni
kuendelea na masomo, Wizara bado haijaweka sera juu ya jambo hili,’’alisema
Masungwa.
Alisema
kuwa agizo la Mkuu wa Wilaya ni gumu utekelezaji wake hivyo utaratibu uliopo wa
kubaki majumbani baada ya kupata ujauzito ndio unaoendelea.
Kwa upande
wake Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mrisho Malaka
alieleza kuwa ipo sheria inayosema kuwa mwanafunzi anayeanza shule
lazima amalize shule kwa mjibu wa sheria ya elimu ya mwaka 1978 pamoja na
kanuni ya Elimu ya Mwaka 2003 pia sheria hiyo inasimamiwa na mabaraza ya Kata
ambapo adhabu zinatolewa huko.
Awali
katika Kikao hicho cha Baraza la Madiwani Diwani wa Viti Maalum Theodora Kisesa
alielezea tatizo la kukithiri kwa utoro na mimba mashuleni kuwa linachangia
kuzorotesha maendeleo ya elimu wilayani humo.
Alisema
kuwa wanafunzi wengi wamekatisha masomo kutokana na kuwa wajawazito na
wanafunzi hao hasa wale waliomaliza elimu ya msingi na kujiunga na sekondari
wamejifungua watoto na wako majumbani hali ambayo inachangia kudorora kwa elimu
kwa wanafunzi wa kike.
Naye
Diwani wa Kata ya Kabungu Selemani Kasonso alieleza kuwa mbali ya mimba pia upo
utoro wa reja reja ambao kwa wingi ambao umekithiri kwa kasi ilhali hakuna hatua zozote za zinazochukuliwa na wazazi kuthibiti
utoro huo pamoja na walimu kujitahidi kuwahimiza wazazi kujali elimu.
Diwani wa
Kata ya Mpanda Ndogo Ahmed Mapengo alihoji utekelezaji wa agizo la Mkuu wa
wilaya hiyo Mwamlima ya kutaka wanaokatiza masomo kwa kuolewa, kuoa au kupata
ujauzito kurejea madarasani mara shule zitakapofunguliwa Mwezi Julai.
Post a Comment