Timu ya
Green City ya Jijini Mbeya imefanikiwa kutwaa kombe la ‘kinywaji kinachotokana
na kampuni ya TBL kinachodhamini mashindano ya timu yenye wachezaji 6 ya safari
ya kuelekea Hispania baada ya kuichabanga Timu ya Savannah kutoka Mkoani Iringa
kwa mabao 8-3.
Michuano
hiyo ambayo ilichezwa katika Viwanja vya City Pub ulikuwa ni wa vuta nikuvute
huku kila upande ukitaka kuchukua ubingwa wa kombe hilo kuungana na timu
zingine nane Jijini Dar es salaam.
Timu itakayoshinda katika timu nane zitakazoshiriki mchuano huyo Leaders Club Jijini Dar es salaam itapata fursa ya kuelekea nchini Hispania kushuhudia ligi ya nchi hiyo.
Mchezo huo
ambao huchezwa kwa dakika 20 na jumla ya wachezaji 6 ulihusisha timu nne kutoka
mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Timu
zilizoshiriki katika mchuano huo ni Green City na White Stars kutoka Jijini
Mbeya,Savannah na Gaddafi kutoka Manispaa ya Iringa.
Green City
ilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Gaddafi mabao
9-0 wakati washindi wa pili Savannah ilifanikiwa kuingia fainali kwa kuifunga
timu ya White Star ya Mbeya mabao 5-3.
Katika
mchezo huo wa fainali magoli ya Green City yalifungwa na Issa Nelson aliyefunga
magoli 3 Castro Litongwale aliyefunga magoli 3 na Lambert Lameck aliyefunga
magoli 2.
Magoli ya
Savannah yalifungwa na Enhard Mgeni magoli 2 na Johnson Ngogo Aliyefunga bao 1.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi Meneja mauzo wa Kinywaji hicho Nyanda za
Juu Kusini Vivianus Rwezaura alisema kuwa atatoa ushirikiano wa hali na mali
kwa washindi ili wafanikiwe kuwa mabingwa wa Castle Lager Perfect 6.
Naye Meneja
wa Kinywaji hicho Kabula Nshimo alisema kuwa mashindano hayo yameleta
changamoto kwa washiriki na kwamba ana imani ushiriki wa timu hizo umeongeza
ari kwa vijana kupenda soka.
Post a Comment