Wajumbe wa ALAT Katavi walipotembelea mradi wa ujenzi wa Bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Kabungu |
Na Kibada Kibada –Katavi.
Wajumbe wa Jumuiya ya serikali za Mitaa tawi la Mkoa wa Katavi
(ALAT) wameshauri serikali kuangalia utaratibu mpya wa sheria za manunuzi
kwa kuwa matumizi ya wakandarasi inachelewesha kazi pamoja na kuchukua
gharama kubwa mno katika utekelzaji wa shughuli.
Ushauri huo ulitolewa na wajumbe hao mara baada ya kutembelea
miradi mbalimbali ya ujenzi wa Maabara,Maktaba na Mabweni yanayojengwa
katika Kata ya Kabungu kwenye shule za sekondari kwa gharama ya Shilingi
milioni 72 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Wajumbe hao walikagua ujenzi wa Bweni na Maabara katika shule ya Sekondari Kabungu kazi iliyofanywa na mafundi wa eneo hilo bila kuwatumia Wakandarasi ambao awali alishindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Awali Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Estoming
Chang’ah.aliwaeleza wajumbe hao kuwa kutokana na muda Halmashauri waliamua
kuwatumia mafundi wa kawaida walioko kwenye eneo husika ili kukamilisha ujenzi
wa maabara baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kukamilika kufuatia
mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kushindwa kukamilisha kandarasi hiyo kwa muda.
Chang’ah alieleza Halmashauri baada ya kupewa agizo
na Mkuu wa Mkoa kuwa maabara zote katika Mkoa zinatakiwa kukamilika
ifikapo mei 30 mwaka huo walilazimika kutafuta fedha na kuwatumia mafundi walioko katika maeneo husika kwa kile kilichoelezwa kuwa iwapo wangetumika wakandarasi kazi
isingeweza kukamilika.
Post a Comment