Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid |
Na Kibada Kibada, Katavi
Mkoa wa
Katavi kupitia sekta ya Afya umewapatia watumishi wa sekta hiyo wapatao 240 mafunzo ya namna ya kutoa huduma ya Tiba ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto.
Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Husein ameeleza kuwa watumishi hao 240 waliopatiwa
mafunzo ni sawa na asilimia 100 ya lengo lililowekwa kuwapatia mafunzo ya huduma hiyo mkoani.
Akifafanua
zaidi Dkt. Husein amesema kuwa hadi kufikia mwezi juni mwaka 2014 jumla ya
vituo 61 sawa na asilimia miamoja na ishirini ya lengo la vituo 51 vinatoa huduma hii katika Mkoa wa
Katavi.
Amesema kuwa
ili kufanikisha adhima ya shirika la
Afya Duniani la kuthibiti maambukizi toka kwa mama mwenye VVU kwenda kwa Mtoto,Wizara ya Afya
ikishirikiana na wadau wa Maendeleo imeanzisha huduma ya Tiba ya kuzuia maambukizi toka kwa Mama mwenye VVU kwenda
kwa Mtoto.
‘’Akina mama
wajawazito wanaonyonyesha wakigundulika kuwa wana maabukizi ya UKIMWI
wataanzishiwa tiba ya kudumu’’alisema.
Aidha kama
Mkoa utahakikisha huduma hii inatolewa katika vituo vyote vinavyotoa huduma ya
Afya ya Uzazi.
Kuhusu
huduma inayotolewa
amesema ni bora ,timu ya Afya Mkoa
na Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo katika sekta ya
Afya Walter Reed zitaendelea kufanya ufuatiliaji na usimamizi elekezi kila
mwezi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Ufundi wa Programu ya Shirika la Walter Reed Dkt Joseph Chintowa ameeleza kuwa
Shirika lake kwa kushirikiana na wadau
wa wote wa Mkoa,Wilaya,Halmashauri na Mji wa Mpanda wanasaidia juhudi za
Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Dkt Chintowa
ametoa wito kwa akina Baba kupima afya pamoja na wake zao ili kujenga familia zenye afya bora na ya uhakika,ambapo
pia amewaasa wazazi kukumbuka dhamana waliyonayo juu ya kuwakinga watoto wao na
maambukizi ya UKIMWI.
Post a Comment